CECH AWAAGA CHELSEA KWA BARUA YA HUZUNI, ISOME HAPA…
Baada ya kumwaga wino kujiunga na
Arsenal, Cech ameandika barua ya kuwaaga mashabiki wa Chelsea kwa
ushirikiano waliompa kwa kipindi chote alichokuwa anaitumikia klabu
hiyo.
Hii hapa ni barua yake….
Sikuwahi kufikiria kama ingekuja
kutokea sikumoja nitakuja kusema kwaheri kwenye klabu ya Chelsea. Klabu
ambayo ilikuwa moyoni kila sekunde tangu nilipojiunga nayo Julai 2004,
timu ambayo nifikiri siku moja ningetukika glovu na viatu vyangu na
kumaliza safari yangu ya soka nikiitumikia. Lakini mara zote maisha
hayako kama unavyofikiria.
Tangu 2004 imekuwa ni safari ya
aina yake yenye mafanikio kuliko changamoto, tumeweza kushinda kila aina
ya taji lililopo kenye ligi ya England hali kadhalika yale ya Ulaya na
lile kubwa kuliko la vilabu bingwa barani Ulaya. Nikitazama nyuma kwenye
mafanikio pamoja na msimu wa 2010, nyuma zaidi kwenye mataji ya 2005 na
2006, ushindi wa vikombe viwili cha EPL na FA najivunia sana hilo.
Pamoja kama timu tuliandika historia.
Majira ya kiangazi ya msimu
uliopita, mambo yalibadilika na nikaelewa sikuwa tena chaguo la kwanza
kwenye nafasi ya golikipa lakini nikahisi haikuwa muda muafaka wa mimi
kuondoka. Wakati ligi inaendelea ilidhihirika wazi kwamba, hali yangu
haingeweza kubadilika na hapo ndipo ninaamini kwa kiwango changu sio mtu
wa kuendelea kukaa benchi. Nikafanya maamuzi ya kuondoka kwenda sehemu
nyingine kutafuta changamoto mpya.
Kukosa nafasi ya kucheza kulinipa
nafasi ya kutuliza akili yangu na kulinifanya nitambue ni kwa kiasi
gani nilikuwa nikifurahia kucheza soka kwa kiwango cha juu, kwasababu
nafasi hiyo niliikumbuka mno kila mechi ambayo sikupangwa. Nimejitoa
kwenye mhezo wa soka na nina njaa ya mafanikiokama ilivyokua tangu
mwanzo na ninapenda changamoto zinazoletwa na wachezaji wengine wenye
viwango vya hali ya juu ninaokutana nao kwenye Premier League ligi bora
na yennye ushindani wa hali ya juu duniani.
Ndio maana niliongea na Bwana
Abramovich kuhusu mimi kuendelea kubakia kwenye ligi hii na ninapenda
kumshuku toka kwenye uvungu wa moyo wangu kwa ushirikiano alionipa juu
ya jambo hili. Inamaana sana kwangu kwasababu bila yeye klabu ya Chelsea
isingefika ilipo sasa. Anastahili pongezi nyingi kwa kile alichoifanyia
klabu na sisi sote kwa ujumla.
Ninamshukuru kila mmoja
anayehusika na klabu ya Chelsea kwa ushirikiano wake, wachezaji,
uongozi, benchi zima la ufundi na makocha wote ambao nilifanyanao kazi
kwa miaka yote. Bila wao isingewezekana kwetu sote kufikia mafanikio
hayo.
Lakini shukrani za dhati
ziwaendee mashabiki wote wa Chelsea. Nilifanya kilakitu kwa ajili yenu
na ninyi mlirudisha upendo wenu kwangu. Sitosahau kitu hicho kamwe. Kita
kaa ndani yangu milele. Tutakutana tena lakini kwa wakati huu
nitasimama kwenye goli lingiine. Ninahakika mtaikumbuka historia na
kuelewa ni muda sasa wa mimi kuanza maisha mapya.
Ninamtakia kilalakheri kila mmoja
kwenye klabu ya Chelsea na nawatakia kilalakheri kwenye msimu mpya ujao
na baadae. Asanteni sana kwa miaka 11 ya miujiza.
Petr Cech.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni