NEWCASTLE INATAKA KUMPOTEZA PAPISS CISSE
Mchezaji wa Senegal ambae alihamia St James Park mwaka 2012 akitokea Freiburg kwa ada ya pound million 9 hayupo sehemu nzuri kuendelea na clun yake ya Newcastle. Tangu ajiunge na club hiyo amefunga magoli 11 kwenye mechi 22.
Kama unakumbuka huyu jamaa aliingia kwenye ugomvi na Jonny Evans na kutemeana mate uwanjani kwenye mechi kati ya Manchester united Vs Newcastle. Baada ya hapo akafungiwa mechi 7 na Newcastle ikapoteza michezo mingi sana wakati yeye hayupo.
Hivi sasa Newcastle wanajiandaa kumsepesha Cisse lakini jamaa anaomba kubaki St James Park ilionyeshe tena kwa kocha wake Steve McClaren kwamba bado anataka kuitumikia club hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni