tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

22 Juni 2015

WBA-UKIMTAKA MZAWA WA BUJUMBURA SAIDO BERAHINO WEKA PAUNI MILIONI 30 MEZANI!

Saido-BerahinoWest Bromwich Albion wanadai Dau la Pauni Milioni 30 ndio waanze kuzungumza na Klabu yeyote inayotaka kumchukua Straika wao mahiri Saido Berahino.
Berahino, Mzaliwa wa Bujumbura, Burundi mwenye Miaka 21 ambae alikulia Uingereza, sasa anaichezea Timu ya Taifa ya England baada ya kuanza kuvichezea Vikosi vya Vijana vya Nchi hiyo kuanzia vile vya U-16 na kupanda hadi kuichezea Timu ya Kwanza.
Hivi sasa Berahino na WBA wana mvutano kuhusu Mkataba mpya ambao Straika huyo amegoma kusaini huku akiwa amebakiwa na Miaka Miwili katika Mkataba wake wa sasa.
Hadi sasa, Berahino anaviziwa na Klabu za Newcastle, Tottenham, Arsenal, Man City na Chelsea.
Klabu nyingine ambayo ina nia ya kumsaini Berahino ni Liverpool lakini hili lina utata na litakuwa gumu kwa vile Wakala wa Mchezaji huyo ni Aidy Ward ambae pia ni Wakala wa Raheem Sterling wa Liverpool na tayari Wady ana bifu kubwa sana na Liverpool kiasi cha kutangaziana vita kuhusu sakata la Sterling kugomea Mkataba mpya na kushikilia kuhama.
Msimu wa 2014/15, Berahino ameifungia WBA Mabao 20.

Hakuna maoni: