MCHEZAJI AME-PROPOSE KWA DEMU WAKE AKISHANGILIA GOLI LAKE
Kila mchezaji ana style yake ya kushangilia goli, wengi wanaruka sarakasi na wengine wanacheza samba. Sasa hii imekua kali zaidi pale jamaa alipotupia nyavuni na kutoa kitambaa chenye maneno akimwambia girlfriend wake kwamba anataka kumchumbia.
Kwenye hiyo mechi mchezjaji huyu wa Colombia baada ya kufunga goli alikimbilia kwenye camera na kutoa kitambaa chenye maneno hayo ambayo alimuomba msichana wake Katya akubali kuolewa na yeye. Habari nzuri ni kwamba msichana huyo alikubali ombi hilo.
Mchezaji Martin Arzuaga alifanya hivyo kwenye mechi kati ya Alianza Petrolera walivyocheza dhidi ya Boyaca Chico na mechi kuisha kwa Alianza kushinda goli 1 kwa bila
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni