MOURINHO AUNGAMA-"HUU NI MWANZO MBOVU MNO!"
Mourinho ameeleza: "Pointi 4 kwa Mechi 4 ni mwanzo mbovu mno!"
Msimu uliopita walipotwaa Ubingwa, Chelsea walishinda Mechi zao zote 4 za kwanza lakini safari hii wametoka Sare 1, Ushindi 1 na Kufungwa 2.
Mourinho amesema: "Ingekuwa Ligi nyingine ningesema Ubingwa basi. Lakini kwa Ligi Kuu England sisemi Ubingwa basi!"
Meneja huyo machachari amekataa kueleza nini tatizo la Kikosi chake mbali ya kukiri wapo baadhi ya Wachezaji wapo chini ya kiwango.
Hata hivyo, Lejendari wa Holland, Ruud Gullit, ambae aliwahi pia kuwa Meneja wa Chelsea kati ya 1996 na 1998, ameeleza: "Kwa sasa Chelsea hawachezi vizuri. Hilo linatokana na upinzani kubaini udhaifu wao. Huo upo upande wa kulia hasa kwa Branislav Ivanovic ambako mashambulizi mengi yanapita."
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni