BAADA FIFPRO KUIPELEKA FIFA MAHAKAMANI KUHUSU UHAMISHO WA WACHEZAJI, MGAWANYIKO WAIBUKA!
PFA imesema kuwa ingawa inaunga mkono nia ya Fifpro kuhusu kupinga Sheria za Uhamisho wa Wachezaji za FIFA, uamuzi wa kwenda Mahakamani ni kulitoa suala hilo nje ya Soka na ipo hatari likakwama na kuchelewesha kuleta mabadiliko na uboreshaji wa hali za Wachezaji.
Uamuzi wa Fifpro kulipeleka suala la Uhamisho wa Wachezaji Mahakamani unatokana na imani yao kuwa Sheria zake zinakiuka Sheria za Ushindani za Jumuia ya Ulaya.
Fifpro, ambacho kinawakilisha zaidi ya Wachezaji wa Kulipwa 65,000 toka Nchi 65 Duniani, kimekuwa na mazungumzo ya Miaka mingi na FIFA, UEFA na Klabu Barani Ulaya ili kuleta mabadiliko kwenye mfumo wa Uhamisho wa Wachezaji lakini mazungumzo hayo yakavunjika Mwezi Januari.
+++++++++++++++++++++++++++++
Fifpro-Mabadiliko wanayotaka:
-Mchezaji yeyote ambae hajalipwa na Klabu yake kwa zaidi ya Siku 30 aruhusiwe kuvunja Mkataba wake ili mradi atoe Notisi ya Maandishi ya Siku 10 kwa Klabu yake.
-Ikiwa Klabu itavunja Mkataba na Mchezaji bila sababu ya haki au Mchezaji akivunja Mkataba na Klabu kwa kutolipwa, Mchezaji alipwe fidia yote na Klabu kwa muda wake wote wa Mkataba.
-Mchezaji yeyote akiwa hana tena Mkataba kufuatia mambo ya hapo juu basi aruhusiwe kujiunga na Klabu nyingine mara moja bila kungojea kufunguliwa kwa Dirisha la Uhamisho kufunguliwa rasmi.
-Mabadiliko yote haya yahusishe Uhamisho wa Wachezaji wa Ndani ya Nchi zao na ule wa Kimataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni