CHELSEA WAIPIGA MTU 9 ARSENAL!
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 19
Chelsea 2 Arsenal 0
1700 Aston Villa v West Brom
1700 Bournemouth v Sunderland
1700 Newcastle v Watford
1700 Stoke v Leicester
1700 Swansea v Everton
1930 Man City v West Ham
++++++++++++++++++++++
Baada ya kuanza ovyo kwa kufungwa Mechi 3, Sare 1 na Kushinda 1 tu na kujikuta wako Nafasi ya 17 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Man City, Leo Chelsea walikamia ushindi na Diego Costa alihakikisha hilo baada ya kuwachokoza Mabeki wa Arsenal na kusababisha Sentahafu wao apande jazba na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Katika Dakika ya 44 ilizuka purukushani kati ya Diego Costa wa Chelsea na Laurent Koscielny wa Arsenal na Costa kuonekana kumpiga Koscielny kisha kumusukuma kwa Kifua hadi chini lakini, kwa mshangao mkubwa, Refa Mike Dean hakumwadhibu Costa kama ilivyotegemewa na badala yake kuwapa Kadi za Njano Costa na Sentahafu wa Arsenal anaetoka Brazil Gabriel.
Dakika moja baadae Gabriel alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kumrushia teke Costa.
Hadi Haftaimu, Chelsea 0 Arsenal 0.
Kipindi cha Pili Dakika ya 53, Frikiki ya Fabregas iliunganishwa kwa Kichwa na Kurt Zouma na kuwapa Chelsea Bao.
Dakika ya 79, Arsenal walibaki Mtu 9 baada ya Kiungo wao Santi Cazorla kupewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Eden Hazard aliipa Chelsea Bao lao la pili katika Dakika ya 91 baada ya Shuti lake kumbabatiza Alex Oxlade-Chamberlain na kutinga.
VIKOSI:
Chelsea: Begovic; Ivanovic, Zouma, Cahill, Azpilicueta; Matic, Fabregas; Pedro, Oscar, Hazard; Diego Costa
Akiba: Blackman, Terry, Mikel, Ramires, Loftus-Cheek, Falcao, Remy.
Arsenal: Cech; Bellerin, Gabriel, Koscielny, Monreal; Coquelin, Cazorla; Ramsey, Ozil, Sanchez; Walcott
Akiba: Ospina, Debuchy, Gibbs, Chambers, Arteta, Oxlade-Chamberlain, Giroud.
REFA: Mike Dean
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumapili Septemba 20
1530 Tottenham v Crystal Palace
1800 Liverpool v Norwich
1800 Southampton v Man United
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni