ENGLAND WIKIENDI-JUMAMOSI SPURS KUANZA NA CITY, MOURINHO AENDELEA KUMSAKAMA WENGER!
Mechi ya kwanza ya Ligi Jumamosi ni huko White Hart Lane Jijini London wakati Tottenham wakiwa Wenyeji wa Vinara wa Ligi Kuu England Man City hapo Saa 8 Dakika 45 Mchana.
City, ambao wanaongoza Ligi wakiwa Pointi 2 mbele ya Man United, wanatinga kwenye Mechi hii wakitoka kupokea kipigo chao cha kwanza cha Ligi Msimu huu wakiwa kwao Etihad Wikiendi iliyopita baada ya kuchapwa 2-1 na West Ham.
Lakini kwa Tottenham wanaingia Mechi hii baada ya kuifunga Crystal Palace 1-0 Wikiendi iliyopita na kuchapwa na Arsenal 2-1 Juzi kwenye Kombe la Ligi.
Hata hivyo, Tottenham hawana rekodi nzuri dhidi ya City baada ya kuchapwa mara 8 katika Mechi 9 zilizopita za Ligi.
Baada ya Mechi hiyo ya awali zitafuata Mechi 6 zitakazoanza Saa 11 Jioni ambapo Timu ya Pili kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England, Man United, watakuwa kwao Old Trafford kucheza na Sunderland ambayo ipo mkiani.
Mechi nyingine za wakati huo huo ni zile za Anfield ambapo Kikosi cha Brendan Rodgers anaesakamwa kwa matokeo mabovu ya Timu yake Liverpool kucheza na Anfield wakati Arsenal watakuwa wageni wa Leicester City.
Mechi ya mwisho kwa Jumamosi ni ile ya kule Saint James Park ambayo Kikosi cha Steve McLaren cha Newcastle yenye matokeo mabovu kabisa kitacheza na Mabingwa Watetezi Chelsea chini ya Meneja wao Jose Mourinho anaeanza kuweweseka kwa mambo kwenda mrama kwake.
Kwenye Ligi Kuu England hivi sasa, Chelsea wapo Nafasi ya 15 na Newcastle wapo Nafasi ya 19 wakiwa wa pili toka mkiani.
Katika hatua ya kushangaza, na pengine ni kutokana na Straika wake Diego Costa kufungiwa Mechi 3 na FA na hapo hapo Beki wa Arsenal Gabriel Paulista kufutiwa Kadi Nyekundu kufuatia mfarakano wao wa Mechi ya Jumamosi iliyopita ambayo Chelsea waliifunga Arsenal 2-0, Mourinho hii Leo ameamua kumpiga madongo Wenger bila kutaja Jina lake.
Akiongea na Wanahabari hii Leo kuhusu Mechi yao ya Ligi inayowakabili, Jose Mourinho alisema: “Nadhani katika Nchi hii yupo Meneja mmoja tu ambae hayuko kwenye presha. Steve McClaren yuko kwenye presha, mimi niko kwenye presha, Brendan Rodgers yuko kwenye presha, Manuel Pellegrini yuko kwenye presha.”
Aliongeza: “Hatupaswi kufungwa Mechi, hatutakiwa kuwa chini ya kiwango. Yupo mmoja hayupo kwenye Listi hiyo. Ni safi kwake. Anaweza kuzungumzia Marefa kabla ya Mechi, anaweza kuzungumzia Marefa baada ya Mechi, anaweza kusukuma Watu kwenye eneo la Ufundi Uwanjani, anaweza kulia asubuhi, kulia jioni, hakuna litakalotokea.”
Mourinho alimalizia kwa kudai Meneja huyo anaweza asishinde lolote lakini akabaki kazini akiwa bado Mfalme kwa vile ana haki maalum.
Mourinho alikataa kumtaja Wenger, ambae amekuwa Meneja wa Arsenal kwa Miaka 19 na hajatwaa Ubingwa wa England tangu 2004, na kujibu: “Mnamjua ni nani!”
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Ligi Kuu England:
**Saa za Bongo
Jumamosi Septemba 2
1445 Tottenham v Man City
1700 Leicester v Arsenal
1700 Liverpool v Aston Villa
1700 Man United v Sunderland
1700 Southampton v Swansea
1700 Stoke v Bournemouth
1700 West Ham v Norwich
1930 Newcastle v Chelsea
Jumapili Septemba 27
1800 Watford v Crystal Palace
Jumatatu Septemba 28
2200 West Brom v Everton
MSIMAMO:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni