TOP 10 YA WACHEZAJI WAKALI AMBAO HAWAJAWAHI KUTWAA BALLON d’Or
10. Arjen Robben
Ameshashinda mataji yote isipokuwa kombe la dunia ambalo timu yake ilishika nafasi ya pili mwaka 2010 nchini Afrika Kusini na wakawa watatu mwaka 2014 nchini Brazil. Jina lake limekuwa likorodheshwa mara kadhaa kwenye orodha ya kuwania mchezaji bora wa dunia FIFA Ballon d’Or lakini hajawahi kutwaa uzo hiyo.
Ni aina ya mchezaji ambaye inapendeza kumtazama na huenda tukalitambua hilo baada ya kumaliza muda wake wa kucheza soka miaka michache ijayo.
Medali ambazo Robben ameshatwaa hadi sasa
- Eredivise title
- Premier League title x2
- FA Cup
- Football League Cup x2
- La Liga title
- Bundesliga title x 3
- DFB- Pokal x 3
- Champions League
- UEFA Super Cup
- World Club Cup
9. Alessandro Del Piero
Kitu cha kushangaza ni kwamba, hajawahi hata kukaribia kushinda tuzo ya Ballon d’Or. Alitakiwa kushinda tuzo hiyo na wote tunajua hilo.
“Yeye ni tofauti na Zidane, anapenda kucheza, anapenda kutoka moyoni; kati yake na mfaransa (Zinedine Zidane) nasimama upande wake”, Diego Maradona.
8. Steven Gerrard
Alicheza kwa moyo wakati yupo Liverpool na hakuona haya kuonesha wazi mapenzi yake kwa klabu yake. Ukiangalia kwenye makabrasha ya rekodi huoni jina lake kwenye orodha ya wachezaji waliowahi kutwaa tuzo kubwa.
“Amekuwa mchezaji mwenye ushawishi mkubwa England”, Sir Alex Ferguson.
“Kwa kazi aliyoifanya, ni miongoni mwa mashujaa”, Ronaldinho.
Mataji aliyoshinda Gerrard akiwa Liverpool
- FA Cup: 2001,2006
- Football League Cup: 2001,2003,2012
- FA Community Shield: 2006
- UEFA Champions League: 2005
- UEFA Cup: 2001
- UEFA Super Cup: 2001,2005
7. Raul Gonzalez
Ameifungia timu ya taifa ya Hispania magoli 40, ameshinda UEFA Champions League mara tatu. Hakuwa mchezaji mwenye mambo mengi uwanjani lakini mafanikio yake yalitosha kumfanya ashinde tuzo hiyo.
“Nataka nimtakie nahodha kila lakheri kwasababu alikuwa nguzo ya mafanikio kwa watu wengi na timu, na amekuwa mtu ambaye watu wengi wanatakiwa kumtazama kwasababu alichokifanya na alichokiamini. Asante kwake na kwa timu, na nakutakia mema kwenye career yako”, David Beckham.
Medali za Raul akiwa Real Madrid
- Intercontinental Cup: 1998, 2002
- UEFA Champions League: 1997–98, 1999–2000, 2001–02
- UEFA Super Cup: 2002
- La Liga: 1994–95, 1996–97, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08
- Supercopa de España: 1997, 2001, 2003, 2008
6. Peter Schmeichel
Rekodi za Henry zinafahamika sana. Bado ni mchezaji pekee aliyehinda mara nyingi kiatu cha dhahabu kwenye EPL. Mshindi mara tano wa tuzo ya chezaji bora wa Ufaransa, mfungaji wa muda wote wa Arsenal, mchezaji mwenye magoli mengi kwenye timu ya Ufaransa, na mshindi mara tatu wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya FWA.
4. Paul Scholes
Lakini tayari mkongwe huyo hayupo tena kwenye soka la ushindani na sehemu pekee unayoweza kumuona ni kwenye uwanja wa mazoezi au kwenye majukwaa ya viwanja akiwa kama mtazamaji.
“Kati ya wachezaji wote wa Manchester United, ningemchagua Scholes-ni kiungo bora wa kizazi hiki. Ningefurahi kucheza pamoja nae”, Pep Guardiola.
Medali alizowahi kutwaa Scholes
- Premier League (11): 1995–96, 1996–97, 1998–99, 1999–2000, 2000–01, 2002–03, 2006–07, 2007–08, 2008–09, 2010–11, 2012–13
- FA Cup (3): 1995–96, 1998–99, 2003–04
- Football League Cup (2): 2008–09, 2009–10
- FA Community Shield (5): 1996, 1997, 2003, 2008, 2010
- UEFA Champions League (2):1998–99, 2007–08
- Intercontinental Cup (1): 1999
- FIFA Club World Cup (1): 2008
3. Paolo Maldin
Alishika namba tatu tena mwaka 2003 wakati huu akishindwa na Pavel Nedved. Ni aibu kwamba
Makombe ambayo Maldini ametwaa akiwa AC Milan
- Serie A (7): 1987–88, 1991–92, 1992–93, 1993–94, 1995–96, 1998–99, 2003–04
- Coppa Italia (1): 2002–03
- Supercoppa Italiana (5): 1988, 1992, 1993, 1994, 2004
- European Cup/Champions League (5): 1988–89, 1989–90, 1993–94, 2002–03, 2006–07
- UEFA Super Cup (5): 1989, 1990, 1994, 2003, 2007
- Intercontinental Cup (2): 1989, 1990
- FIFA Club World Cup (1): 2007
2. Ryan Giggs
Alilipendezesha soka la England katika historia ya soka. Alicheza mechi 963 akiwa na Manchester United akifanikiwa kushinda mataji 34. Sababu za kwanini Giggs hajawahi kushinda tuzo ya Ballon d’Or ni kitendawili ambacho hakijapatiwa majibu hadi sasa.
Watu wengine wanaweza kusema Giggs hana historia nzuri akiwa na timu yake ya taifa lakini wanasau Andriy Shevchenko alitwaa tuzo hiyo mwaka 2004 huku akiwa hana historia hata ya kukaribia kushinda taji lolote akiwa kwenye timu ya taifa.
Mafanikio aliyopata Giggs akiwa Manchester United
- 963 games for Manchester United
- 672 league appearances
- 151 Champions League appearances
- 109 league goals
- 45 opponents in the Premier League
- 34 trophies
- 13 Premier League titles
- 4 FA Cups
- 2 Champions Leagues
- 1 club World Cup
1. Xavi Hernandez
Johan Cruyff: “Kama Xavi asipokuwa sawa basi Barcelona haitacheza vizuri kwa kiwango kilekile kama ilivyozoeleka. Ni mtu ambaye anamiliki na kuamua mchezo. Kucheza kwake kunairuhusu timu kucheza. Yuko tofauti”.
Medali ambazo Xavi amevaa akiwa Barcelona
- La Liga: 1998–99, 2004–05, 2005–06, 2008–09, 2009–10, 2010–11, 2012–13, 2014–15
- Copa del Rey: 2008–09, 2011–12, 2014–15
- Supercopa de España: 2005, 2006, 2009, 2010, 2011, 2013
- UEFA Champions League: 2005–06, 2008–09, 2010–11, 2014–15
- UEFA Super Cup: 2009, 2011
- FIFA Club World Cup: 2009, 2011
- International
- FIFA World Cup: 2010
- UEFA European Football Championship: 2008, 2012
- Summer Olympics Silver Medal: 2000
- FIFA Confederations Cup Silver Medal: 2013
- FIFA World Youth Championship: 1999
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni