tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

22 Juni 2015

NANI ATACHEZA NA NANI ROBO FAINALI YA COPA AMERICA…RATIBA HII HAPA.

Copa-America-2015Michuano ya kombe la mataifa ya America Kusini maarufu kama Copa America imeingia kwenye hatua ya robo fainali baada ya michezo ya Kundi C kumalizika usiku wa kuamkia leo.
Robo fainali ya kwanza itawakutanisha wenyeji wa michuano hiyo timu ya Chile itakuwa ikikipiga dhidi ya Uruguay siku ya Jumatano, Chile watahitaji ushindi kwa nguvu zote kwasababu wao ndio wenyeji wa michuano hivyo watataka kuhakikisha wanafika mbali kwenye mashindano hayo wakiwa kwenye ardhi ya nyumbani wakiongozwa na nyota wao wa Arsenal Alexis Sanchez na kiungo wa Juventus Aturo Vidal.
Lakini Cavani, Godin na nyota wengine wengi wa Uruguay watakuwa tayari kuwakabili Chile kwenye mchezo huo wa robo fainali ya kwanza.
Bolivia wao watakipiga dhidi ya Peru kwenye robo fainali ya pili itayochezwa siku ya Alhamisi. Bolivia imewashangaza wengi kwa kutinga kwake hatua ya robo fainali kwasababu wengi walikuwa wakiibeza na kutoipa nafasi kwenye michuano ya mwaka huu. Lakini mshambuliaji wa Bayern Munich Claudio Pizarro anatarajiwa kukiongoza kikosi cha Peru kuikabili Bolivia.
Mchezo mwingine utakaovuta hisia za watu wengi ni ule ambao Argentina itakapochuana na Colombia kwenye robo fainali ngumu na ya kukata na shoka itakayopigwa siku ya Ijumaa.
Nyota wa klabu ya Barcelona Lionel Messi atakuwa akiwaongoza nyota wengine kama Di Maria, Aguero, Tevez na wengine wengi kutafuta ushindi mbele ya Colombia ambayo inaongozwa na nyota wa Madrid James Rodriguez na wenzake kama Cuadrado na Falcao.
Brazil watakipiga dhidi ya Paraguay kwenye robo fainali ya mwisho itakayochezwa Jumamosi. Brazil bado itaendelea kumkosa Neymar na itakuwa ikitupa karata yake ya pili kujaribu kutafuta ushindi bila nyota huyo aliyefungiwa mechi nne.
Ratiba kamili ya robo fainali hii hapa;
Chile v Uruguay – Jumatano
Bolivia v Peru – Alhamisi 
Argentina v Colombia – Ijumaa
Brazil v Paraguay – Jumamosi

JEURI YA REAL, KIBURI CHA MAN UNITED-UNAMTAKA DE GEA, TUPE RAMOS!

SERGIO-RAMOSNi wazi imeibuka vita ya chini kwa chini kati ya Vilabu vikubwa Barani Ulaya, Real Madrid na Manchester United, David-de-Gea-shangiliasakata ambalo lilianza kwa Real kumtaka Kipa wa Man United David de Gea.
Akiwa amebakisha Mwaka mmoja kwenye Mkataba wake na Man United, David de Gea alipewa Mkataba mpya ulioboreshwa lakini akawa anasita kuusaini na kuibuka ripoti kuwa anataka kurudi kwao Spain kuidakia Real Madrid.
Wakati hilo likonekana halikwepeki Man United nao wakajibu mapigo kwa kuripotiwa wakitaka dili yeyote ya David de Gea ihusishe na wao kupewa Mchezaji na sasa Beki Sergio Ramos ndie ameibuka mlengwa.
Lakini habari za ndani ya Real zinadai Ramos hawezi kwenda kokote kwa vile Mkataba wake wa sasa unaoisha 2017 una kipengele cha Real kulipwa Euro Milioni 200 ikiwa atahama kabla Mkataba kwisha.
Vile vile, Real wanaamini wao watampata De Gea na Ramos hataenda kokote kwa vile nia yake si kuhama bali ni kuboreshewa Mkataba wakati De Gea anataka kuhama ili arudi kwao.
Hata hivyo, Real wanasemekana kukiri kuwa mambo ni magumu kwani Man United hawataki mazungumzo yeyote kwa wakati huu.

COPA AMERICA: BRAZIL BILA NEYMAR YATINGA ROBO FAINALI, FIRMINO SHUJAA!

COPA-AMERICA15Brazil, wakicheza bila ya Kepteni wao Neymar aliefungiwa Mechi 4, wametinga Robo Fainali ya Copa America baada ya kuifunga Venezuela 2-1 hapo Jana huko Estadio Municipal Concepcion Mjini Concepcion Nchini Chile.
Ushindi huo umeipa Brazil ushindi wa Kundi C na sasa watacheza na Paraguay, waliomaliza Nafasi ya Pili toka Kundi B, katika Robo Fainali.
Bao za Brazil katika Mechi hii na Venezuela zilifungwa na Thiago Silva, Dakika ya 9, na Roberto Firmino, Dakika ya 51 wakati lile la Venezuela lilifungwa na Nicolas Fedor Miku katika Dakika ya 84.
Katika Mechi nyingine ya Kundi C, Colombia na Peru zilitoka 0-0 na zote kutinga Robo Fainali.
++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
KUNDI A
**Kila Timu imecheza Mechi 3
1 Chile Pointi 7
2 Bolivia 4
3 Ecuador 3
4 Mexico 2
KUNDI B
**Kila Timu imecheza Mechi 3
1 Argentina Pointi 7
2 Paraguay 5
3 Uruguay 4
4 Jamaica 0
KUNDI C
**Kila Timu imecheza Mechi 3
1 Brazil Pointi 6
2 Peru Pointi 4
3 Colombia 4
4 Venezuela 3 
**Timu 2 za Juu kila Kundi na Timu za 3 mbili Bora zitasonga Robo Fainali
++++++++++++++++++++++
Robo Fainali zitaanza kuchezwa hapo Jumatano kwa Mechi kati ya Mabingwa Watetezi Uruguay na Wenyeji Chile.
VIKOSI:
Brazil (Mfumo 4-2-3-1): Jefferson; Dani Alves, Thiago Silva, Miranda, Filipe Luis; Fernandinho, Elias; Willian, Coutinho, Robinho; Firmino.
Akiba: Neto, Marcelo Grohe, Fabinho, Marquinhos, David Luiz, Geferson, Casemiro, Fred, Douglas Costa, Everton Ribeiro, Diego Tardelli.
Venezuela (Mfumo 4-2-3-1): Baroja; Rosales, Tunez, Vizcarrondo, Cichero; Rincon, Seijas; Guerra, Arango, Vargas; Rondon.
Akiba: Hernandez, Farinez, Angel, Martinez, Acosta, Perozo, Murillo, Gonzalez, Lucena, Rivas, Miku.
REFA: Enrique Cáceres [Paraguay]
FIRMINO-SCORES-COPA
COPA AMERICA 
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Alhamisi Juni 11
KUNDI A Chile 2 Ecuador 0
Ijumaa Juni 12
KUNDI A Mexico 0 Bolivia 0
Jumamosi Juni 13
KUNDI B Uruguay 1 Jamaica 0
KUNDI B Argentina 2 Paraguay 2
Jumapili Juni 14
KUNDI C Colombia 0 Venezuela 1
KUNDI C Brazil 2 Peru 1
Jumatatu Juni 15
KUNDI A Ecuador 2 Bolivia 3
KUNDI A Chile 3 Mexico 3
Jumanne Juni 16
KUNDI B Paraguay 1 Jamaica 0
KUNDI B Argentina 1 Uruguay 0
Jumatano Juni 17
KUNDI C Brazil 0 Colombia 1
Alhamisi Juni 18
KUNDI C Peru 1 Venezuela 0
Ijumaa Juni 19
KUNDI A Mexico 1 Ecuador 2
KUNDI A Chile 5 Bolivia 0
Jumamosi Juni 20
KUNDI B Uruguay 1 Paraguay 1
KUNDI B Argentina 1 Jamaica 0
Jumapili Juni 21
KUNDI C Colombia 0 Peru 0 
KUNDI C Brazil 2 Venezuela 1
ROBO FAINALI
Jumatano Juni 24
Chile v Uruguay (Saa 8 na Nusu Usiku)
Alhamisi Juni 25
Bolivia v Peru (Saa 8 na Nusu Usiku)
Ijumaa Juni 26
Argentina v Colombia (Saa 8 na Nusu Usiku)
Jumamosi Juni 27
Brazil v Paraguay (Saa 6 na Nusu Usiku)
NUSU FAINALI
Jumatatu Juni 29
RF1 v RF2 (Saa 8 na Nusu Usiku)
Jumanne Juni 30
RF3 v RF4 (Saa 8 na Nusu Usiku)
MSHINDI WA 3
Ijumaa Julai 3
(Saa 8 na Nusu Usiku)
FAINALI
Jumamosi Julai 4
(Saa 5 Usiku)

EUROPA LIGI: DROO YA RAUNDI YA KWANZA TAYARI, WEST HAM KUCHEZA NA FC LUSITANS YA ANDORRA!

EUROPALIGI-NICE-2Droo za Mechi  za Raundi ya Kwanza ya Mtoano na ile ya Pili za EUROPA LIGI kwa ajili ya Msimu mpya wa 2015/15 zimefanyika Leo huko Nyon, Uswisi na kuhusisha Klabu 102 ambazo ni nyingi kupita wakati wowote.
West Ham ya England, ambayo ilimaliza Ligi Kuu England ikiwa Nafasi ya 12 na kuingizwa EUROPA LIGI kwa sababu ya kuongoza Tebo ya Uchezaji wa Haki, itacheza na FC Lusitans ya Andorra katika Raundi ya Kwanza ya Mtoano.
Mshindi wa Mechi hii atatinga Raundi ya Pili ya Mtoano na kucheza na Mshindi kati ya Birkirkara FC ya Malta na Ulisses FC ya Armenia.
RAUNDI YA KWANZA YA MTOANO
**Mechi kuchezwa Julai 2 na Marudiano Julai 9
Víkingur Reykjavík (ISL) v NK Koper (Slovenia)
Newtown AFC (WAL) v Valletta FC (MLT)
Glenavon FC (NIR) v FC Shakhtyor Soligorsk (BLR)
NSÍ Runavík (FRO) v Linfield FC (NIR)
FK Atlantas Klaipėda (LTU) v PFC Beroe Stara Zagora (BUL)
FK Spartaks Jūrmala (LVA) v FK Budućnost Podgorica (MNE)
FC Progrès Niederkorn (LUX) v Shamrock Rovers FC (IRL)
Cork City FC (IRL) v KR Reykjavík (ISL)
University College Dublin AFC (IRL)* v F91 Dudelange (LUX)
FC Sheriff (MDA) v Odds BK (NOR)
FC Dinamo Tbilisi (GEO) v Qäbälä FK (AZE)
FC Differdange 03 (LUX) v Bala Town FC (WAL)
Brøndby IF (DEN) v AC Juvenes/Dogana (SMR)
Debreceni VSC (HUN) v FK Sutjeska (MNE)
FK Crvena zvezda (SRB) v FC Kairat Almaty (KAZ)
FC Aktobe (KAZ) v Nõmme Kalju FC (EST)
Go Ahead Eagles (NED)* v Ferencvárosi TC (HUN)
NK Domžale (SVN) v FK Čukarički (SRB)
FK Kukësi (ALB) v FC Torpedo Zhodino (BLR)
KF Renova (MNE) v FC Dacia Chisinau (MDA)
KF Shkëndija (MKD) v Aberdeen FC (SCO)
MTK Budapest (HUN) v FK Vojvodina (SRB)
FC Ordabasy Shymkent (KAZ) v Beitar Jerusalem FC (ISL)
FC Flora Tallinn (EST) v FK Rabotnicki (MKD)
FC Dinamo Batumi (GEO) v AC Omonia (CYP)
FK Trakai (LTU) v HB Tórshavn (FRO)
Glentoran FC (NIR) v MŠK Žilina (SVK)
Alashkert FC (ARM) v Saint Johnstone FC (SCO)
FK Olimpic Sarajevo (BIH) v FC Spartak Trnava (SVK)
Víkingur (FRO) v Rosenborg BK (NOR)
Skonto FC (LVA) v Saint Patrick's Athletic FC (IRL)
Balzan FC (MLT) v FK Željezničar (BIH)
UE Sant Julià (AND) v Randers FC (DEN)
FK Kruoja Pakruojis (LTU) v Jagiellonia Białystok (POL)
KF Laçi (ALB) v İnter Bakı PİK (AZE)
FK Partizani (ALB) v Strømsgodset IF (NOR)
FK Jelgava (LVA) v PFC Litex Lovech (BUL)
FC Lusitans (AND) v West Ham United FC (ENG)*
SJK Seinäjoki (FIN) v FH Hafnarfjördur (ISL)
FC Lahti (FIN) v IF Elfsborg (SWE)
JK Sillamäe Kalev (EST) v HNK Hajduk Split (CRO)
FC Saxan (MDA) v Apollon Limassol FC (CYP)
FC Shirak (ARM) v HŠK Zrinjski (BIH)
VPS Vaasa (FIN) v AIK Solna (SWE)
FK Mladost Podgorica (MNE) v Neftçi PFK (AZE)
NK Celje (SVN) v WKS Śląsk Wrocław (POL)
SP La Fiorita (SMR) v FC Vaduz (LIE)
Birkirkara FC (MLT) v Ulisses FC (ARM)
AUK Broughton FC (WAL) v NK Lokomotiva Zagreb (CRO)
FC Botoşani (ROU) v Tskhinvali (GEO)
Europa FC (GIB) v ŠK Slovan Bratislava (SVK)

EUROPA LIGI: DROO YA RAUNDI YA KWANZA TAYARI, WEST HAM KUCHEZA NA FC LUSITANS YA ANDORRA!

EUROPALIGI-NICE-2Droo za Mechi  za Raundi ya Kwanza ya Mtoano na ile ya Pili za EUROPA LIGI kwa ajili ya Msimu mpya wa 2015/15 zimefanyika Leo huko Nyon, Uswisi na kuhusisha Klabu 102 ambazo ni nyingi kupita wakati wowote.
West Ham ya England, ambayo ilimaliza Ligi Kuu England ikiwa Nafasi ya 12 na kuingizwa EUROPA LIGI kwa sababu ya kuongoza Tebo ya Uchezaji wa Haki, itacheza na FC Lusitans ya Andorra katika Raundi ya Kwanza ya Mtoano.
Mshindi wa Mechi hii atatinga Raundi ya Pili ya Mtoano na kucheza na Mshindi kati ya Birkirkara FC ya Malta na Ulisses FC ya Armenia.
RAUNDI YA KWANZA YA MTOANO
**Mechi kuchezwa Julai 2 na Marudiano Julai 9
Víkingur Reykjavík (ISL) v NK Koper (Slovenia)
Newtown AFC (WAL) v Valletta FC (MLT)
Glenavon FC (NIR) v FC Shakhtyor Soligorsk (BLR)
NSÍ Runavík (FRO) v Linfield FC (NIR)
FK Atlantas Klaipėda (LTU) v PFC Beroe Stara Zagora (BUL)
FK Spartaks Jūrmala (LVA) v FK Budućnost Podgorica (MNE)
FC Progrès Niederkorn (LUX) v Shamrock Rovers FC (IRL)
Cork City FC (IRL) v KR Reykjavík (ISL)
University College Dublin AFC (IRL)* v F91 Dudelange (LUX)
FC Sheriff (MDA) v Odds BK (NOR)
FC Dinamo Tbilisi (GEO) v Qäbälä FK (AZE)
FC Differdange 03 (LUX) v Bala Town FC (WAL)
Brøndby IF (DEN) v AC Juvenes/Dogana (SMR)
Debreceni VSC (HUN) v FK Sutjeska (MNE)
FK Crvena zvezda (SRB) v FC Kairat Almaty (KAZ)
FC Aktobe (KAZ) v Nõmme Kalju FC (EST)
Go Ahead Eagles (NED)* v Ferencvárosi TC (HUN)
NK Domžale (SVN) v FK Čukarički (SRB)
FK Kukësi (ALB) v FC Torpedo Zhodino (BLR)
KF Renova (MNE) v FC Dacia Chisinau (MDA)
KF Shkëndija (MKD) v Aberdeen FC (SCO)
MTK Budapest (HUN) v FK Vojvodina (SRB)
FC Ordabasy Shymkent (KAZ) v Beitar Jerusalem FC (ISL)
FC Flora Tallinn (EST) v FK Rabotnicki (MKD)
FC Dinamo Batumi (GEO) v AC Omonia (CYP)
FK Trakai (LTU) v HB Tórshavn (FRO)
Glentoran FC (NIR) v MŠK Žilina (SVK)
Alashkert FC (ARM) v Saint Johnstone FC (SCO)
FK Olimpic Sarajevo (BIH) v FC Spartak Trnava (SVK)
Víkingur (FRO) v Rosenborg BK (NOR)
Skonto FC (LVA) v Saint Patrick's Athletic FC (IRL)
Balzan FC (MLT) v FK Željezničar (BIH)
UE Sant Julià (AND) v Randers FC (DEN)
FK Kruoja Pakruojis (LTU) v Jagiellonia Białystok (POL)
KF Laçi (ALB) v İnter Bakı PİK (AZE)
FK Partizani (ALB) v Strømsgodset IF (NOR)
FK Jelgava (LVA) v PFC Litex Lovech (BUL)
FC Lusitans (AND) v West Ham United FC (ENG)*
SJK Seinäjoki (FIN) v FH Hafnarfjördur (ISL)
FC Lahti (FIN) v IF Elfsborg (SWE)
JK Sillamäe Kalev (EST) v HNK Hajduk Split (CRO)
FC Saxan (MDA) v Apollon Limassol FC (CYP)
FC Shirak (ARM) v HŠK Zrinjski (BIH)
VPS Vaasa (FIN) v AIK Solna (SWE)
FK Mladost Podgorica (MNE) v Neftçi PFK (AZE)
NK Celje (SVN) v WKS Śląsk Wrocław (POL)
SP La Fiorita (SMR) v FC Vaduz (LIE)
Birkirkara FC (MLT) v Ulisses FC (ARM)
AUK Broughton FC (WAL) v NK Lokomotiva Zagreb (CRO)
FC Botoşani (ROU) v Tskhinvali (GEO)
Europa FC (GIB) v ŠK Slovan Bratislava (SVK)

CRISTIANO RONALDO HANA FURAHA NA AMANI NDANI YA REAL MADRID KWASABABU HII

RON
Kutokana na ripoti za gazeti la AS limeandika kwamba mchezaji muhimu wa Real Madrid Cristiano Ronaldo hana furaha na amani ndani ya Real Madrid hivi sasa.
Sababu kubwa inayomfanya CR7 asiwe na amani na furaha ndani ya Real ni kutokana na club inavyowa-treat marafiki zake wa karibu Iker Casillas na Sergio Ramos.
Licha ya kuwa marafiki zake wa karibu ni kwamba wachezaji hao wameitumikia club hiyo kwa muda mrefu lakini kwa wakati huu Real inataka kwa kuwauza kwa utaratibu ambao wote wawili hawafurahii. Cassilas anaonekana kachoka anatakiwa kubadilishwa na De Gea pamoja na dau la pesa.
Pia Ramos pia mambo yake sio mazuri. Cristiano Ronaldo hafurahii yanayotokea na kikubwa zaidi anahofia na yeye siku moja yasije kumtokea kama haya yanayowatokea wenzake.

DIEGO MARADONA ANATARAJIWA KUTANGAZA NIA

dona
Mkongwe wa soka kutoka nchini Argentina Diego Maradona ambae ana historia kubwa kwenye ulimwengu wa soka kwa uwezo wake mkubwa na pia maisha yake ya nje ya soka kufatiliwa sana na vyombo vya habari.
Kitu kipya kutoka kwa Maradona hivi sasa ni kwamba anatarajiwa kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais wa FIFA.
Hivi sasa inasubiliwa taarifa rasmi kutoka FIFA lini uchaguzi mkuu utafanyika baada ya Blatter kujiuzulu.
Watu mbalimbali wamejitokeza na Maradona amemwambia mwandishi wa habari maarufu wa michezo Victor Hugo Morales kwamba amezungumza na Maradona na amemwambia kwamba atatangaza nia yake ya kugombea urais wa FIFA.
Alijibu kwa maneno machache tu, “I am a Candidate”. Maradona alinijibu hivyo baada ya kumuuliza kuhusu mawazo yake ya kuhusu kugombea nafasi hiyo kubwa kwenye FIFA.
Rais wa Venezuela aliwai kusema kwamba Maradona ndie awe Rais anaefuatia wa FIFA. Maradona ana miaka

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA THIERRY HENRY KUHUSU MESUT OZIL

Siku chache zilizopita Henry alishiriki kwenye uzinduzi wa jezi mpya za Arsenal. Lakini hivi sasa hanbari inayomuweka Titi kwenye headline ni jinsi alivyomsifia sana Mesut Ozil.
ozil
Kwenye kauli yake Henry alitumia maneno mengi kumpa sifa mchezaji huyo wa Arsenal. Kwenye tafsiri yake Henry alisema hivi, “Mesut ni mchezaji mzuri sana, wote tunajua kuhusu uwezo wake. Wote tunajua amefanya nini kwenye mchezo wa soka. Yeye ni bingwa wa dunia na inabidi uheshimu hilo na akiwa kwenye mechi anakuwa vizuri sana. Ni mchezaji wa ajabu. Kama akiwa kwenye fomu aliyoonyesha kwenye FA Cup final basi ni vigumu sana kumzuia kufanya akitakacho”.
Hayo ni maneno ya legend Thierry Henry
ozil2

Dili limetiki: Peter Cech atua Arsenal rasmi

Peter Cech to ArsenalArsenal imekamilisha usajili wa golikipa wa Chelsea Peter Cech na anatarajiwa kukipiga na klabu yake ya zamani akiwa ametinga uzi wa Emirates kwenye mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa Agosti 2 mwaka huu kwenye uwanja wa Wimbley
Habari kamili inakujia hivi punde…..

HII NDIO SIRI YA MASTAA KUVAA JEZI NAMBA 10

RIVA
Lionel Messi anavaa jezi namba 10.
Neymar anavaa jezi namba 10.
Wayne Rooney anavaa jezi namba 10
Washindi wa hivi karibuni wa Ballon d’Or wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Michael Owen, Ronaldinho Gaucho na Ricaldo Kaka wote walikua wakivaa jezi namba 10.
Moja ya kukua kwa umaarufu wa jezi no. 10 ni kuwahi kuvaliwa na wachezaji bora wa muda wote Ulimwenguni, Pele pamoja na Diego Armando Maradona.
Hilo limechangia kwa kiasi kikubwa jezi hii kuwa na mvuto wa aina yake na kupendwa na mastaa wengi wa soka.
Lakini sababu nyingine ambayo ndiyo ilikua chanzo cha Pele na Maradona kuvaa jezi hiyo kubwa kabisa katika soka ilikuwa ni utamaduni wa kawaida wa kupanga first eleven.
Katika kikosi cha wachezaji 11 wa kwanza, jezi ziligawiwa kuanzia yenye namba ndogo kutoka kwa golikipa hadi kwa mchezaji wa misho namba 11 kulingana na nafasi uwanjani.
Hivyo automatic kutokana na position zao, Pele na Maradona wakajikuta wakigawiwa jezi namba 10 kama washambuliaji wa timu zao.
Mfumo wa mpira ulipobadilika na kuwa 4 4 2 uliwafanya washambuliaji wa mbele wawili mmoja kuvaa jezi namba 10 na mwingine namba 9. Hali hii ikasababisha pia jezi namba 9 kuwa pia na umaarufu wa aina yake. Inavaliwa na Luis Suarez, Samuel Eto’o akiwa Barcelona pamoja na Ronaldo De Lima.
Lakini mabadiliko hayo ya jezi yamepelekea wachezaji wengine kuchagua jezi zenye namba kubwa zaidi ya zilizopo ndani ya 11. David Beckham alichagua jezi no.23 alipotua Madrid na amestaafu akivaa hiyo.

NA HII NDIO CLUB ILIYOMNASA ANDREA PIRLO

PPPPPPPPPP
Baada ya kucheza fainali ya UEFA na Juventus hivi sasa ni wakati muafaka kwa legendali Andrea Pirlo kusepa kwenye club hyo na kuanza maisha mapya kwenye club nyingine.
Habari zinaripitiwa kwamba hadi sasa kila kitu kimekaa sawa kwenye makubaliano kati ya yake na New York City FC inayoshiriki kwenye MLS nchini Marekani.
Gazeti maarufu la The New York Post limeandika kwamba dili kubwa limeshakamilishwa japokuwa bado halijatangazwa bado
Pirlo ana miaka 36 na amecheza miaka 10 na AC Milan kabla hajaamia Juventus 2012 na kupata mafanikio zaidi.
Jumamosi iliyopita Pirlo alitumia muda wake kuangalia baseball kwenye uwanja wa Yankees Stadium na inategemewa ijumaa hii Pirlo atatangazwa rasmi

Kunani kati ya Karruache na mchezaji mpya Mshambuliaji mpya wa klabu ya Manchester United Memphis Depay, anaweza kujiingiza kwenye malumbano na muimbaji Chris Brown baada ya jana usiku kupost picha akiwa katika pozi tata na ex girlfriend wa muimbaji huyo, Karrueche Tran.

 Depay ambaye amesajiliwa na United mapema mwezi uliopita, kwa sasa yupo mapumzikoni nchini Marekani ambapo ndio amekutana na Karruache.
Ikumbukwe wiki kadhaa zilizopita mwanamitindo mkongwe Tyson Beckford aliingia kwenye malumbano na muimbaji Chris Brown baada ya mwanamitindo huyo kupost picha ya ‘selfie’ akiwa na mwanadada Karrueche Tran.
Chris Brown amekuwa na kasumba ya kugombana na kila mwanaume ambaye anakuwa na ukaribu na Karrueche, alianza na Drake na kisha Tyson Beckford.
Depay ambaye anatarajiwa kujiunga rasmi na timu yake mpya mapema mwezi ujao, alipost picha hiyo na Karruache na hakuandika caption yoyote huku akiwaacha mashabiki wake wakimsifia kwamba anapendezana na Msichana huyo huku wengine wakimuonya juu ya Chris Brown.

WBA-UKIMTAKA MZAWA WA BUJUMBURA SAIDO BERAHINO WEKA PAUNI MILIONI 30 MEZANI!

Saido-BerahinoWest Bromwich Albion wanadai Dau la Pauni Milioni 30 ndio waanze kuzungumza na Klabu yeyote inayotaka kumchukua Straika wao mahiri Saido Berahino.
Berahino, Mzaliwa wa Bujumbura, Burundi mwenye Miaka 21 ambae alikulia Uingereza, sasa anaichezea Timu ya Taifa ya England baada ya kuanza kuvichezea Vikosi vya Vijana vya Nchi hiyo kuanzia vile vya U-16 na kupanda hadi kuichezea Timu ya Kwanza.
Hivi sasa Berahino na WBA wana mvutano kuhusu Mkataba mpya ambao Straika huyo amegoma kusaini huku akiwa amebakiwa na Miaka Miwili katika Mkataba wake wa sasa.
Hadi sasa, Berahino anaviziwa na Klabu za Newcastle, Tottenham, Arsenal, Man City na Chelsea.
Klabu nyingine ambayo ina nia ya kumsaini Berahino ni Liverpool lakini hili lina utata na litakuwa gumu kwa vile Wakala wa Mchezaji huyo ni Aidy Ward ambae pia ni Wakala wa Raheem Sterling wa Liverpool na tayari Wady ana bifu kubwa sana na Liverpool kiasi cha kutangaziana vita kuhusu sakata la Sterling kugomea Mkataba mpya na kushikilia kuhama.
Msimu wa 2014/15, Berahino ameifungia WBA Mabao 20.

EURO U-21: JESSE LINGARD AIPA USHINDI ENGLAND!


jesse-lingardEngland, wakicheza Mechi yao ya pili ya Fainali za Mashindano ya Mataifa ya Ulaya kwa Vijana chini ya Miaka 21, EURO U-21, Leo wameifunga Sweden 1-0 huko Ander Stadium, Olomouc Nchini Czech Republic.
Katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi B England walifungwa 1-0 na Portugal lakini Leo mkombozi wao alikuwa Jesse Lingard, Chipukizi wa Manchester United, alieingizwa Dakika ya 55 kumbadili Pritchard na kufunga Bao pekee na la ushindi kwa Shuti kali kufuatia Kona.
England watamaliza Mechi yao ya mwisho ya Kundi C kwa kucheza na Italy hapo 
VIKOSI:
Sweden U21: Carlgren, Lindelof, Baffo, Helander, Augustinsson, Khalili, Hiljemark, Lewicki, Tibbling, Guidetti, Thelin
Akiba: Rinne, Hrgota, Zeneli, Ishak, Olsson, Holmen, Larsson, Quaison, Konate, Gustafsson, Linde.
England U21: Butland, Jenkinson, Moore, Gibson, Garbutt, Redmond, Hughes, Chalobah, Pritchard, Carroll, Kane
Akiba: Bond, Forster-Caskey, Stones, Ward-Prowse, Keane, Lingard, Ings, Afobe, Chambers, Targett, Loftus-Cheek, Bettinelli.
REFA: Javier Estrada Fernandez (Spain)
MAKUNDI
KUNDI A
**Kila Timu imecheza Mechi 2
1 Germany Pointi 4
2 Denmark 3
3 Czech Rep 3
4 Serbia 1
KUNDI B
1 Sweden Mechi  2 Pointi 3
2 Portugal Mechi 1 Pointi 3
3 England Mechi 2 Pointi 3
4 Italy Mechi 1 Pointi 0
RATIBA/MATOKEO:
**Mechi zote Saa 3 Dakika 45 Usiku
Jumapili Juni 21
Sweden 0 England 1
Italy v Portugal
Jumanne Juni 23
Czech Republic v Germany
Denmark v Serbia
Jumatano Juni 24
England v Italy
Portugal v Sweden

PETR CECH AIKARIBIA EMIRATES!

Kipa wa Chelsea Petr Cech anakaribia kuhamia Arsenal kwa mpetr-cech-chelsea 3317717ujibu wa ripoti za kuaminika huko England.
Cech, mwenye Miaka 33, ameshaafikiana maslahi yake binafsi na Arsenal na kilichobaki ni kusawazisha mvutano kati ya Chelsea na Arsenal kuhusu Ada ya Uhamisho huku pande hizo mbili zikikubaliana kuendelea na mazungumzo.
Cech amebakiza Mwaka mmoja katika Mkataba wake na Chelsea na ameruhusiwa rasmi na Mmiliki wa Klabu hiyo, Roman Abramovich, kuhamia Klabu yeyote anayotaka baada ya kusugua Benchi Msimu uliopita akiwa Kipa Namba mbili nyuma ya Thibaut Courtois.
Cech alijiunga na Chelsea Mwaka 2004 akitokea Klabu ya France Rennes na kuidakia Chelsea Mechi 333.
Ingawa Cech mwenyewe anapendelea kubakia London na hivyo kujiunga na Arsenal, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho hataki hilo na alipendelea Kipa huyo wa Kimataifa kutoka Czech Republic ahamie kwa Mabingwa wa France Paris Saint-Germain.
Lakini Karata ya Trufu ya Mmiliki Roman Abramovich ndiyo imemtoa kapa Jose Mourinho na kumpa mtaji Kipa Mkongwe Petr  Cech.
 

amos anukia kutua Old Trafford

RamosMachester United wanakaribia kumsajili beki wa Real Madrid Sergio Ramos kwenye uhamisho utakaohusisha kubadilishana wachezaji ambapo Real Madrid watalazimika kumtoa Ramos pamoja na kiasi cha pesa ili kumnasa golikipa namba moja wa Man United David de Gea.
Ramos haelewi ni kwanini Madrid wameanua kumruhusu aondoke wakati bado anamkataba wa miaka miwili na klabu hiyo lakini akawaambia kwamba, iwapo naondoka Madrid basi sehemu pekee anayotaka kwenda ni Manchester United.
Ramos 1Kama United watafanikisha dili la kuondoka kwa De Gea basi watabadilishana golikipa huyo na Ramos ambaye ni mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Hispania kwenye dili kubwa baina ya vilabu hivyo viwili tangu Madrid imsajili Cristiano Ronaldo mwaka 2009.
Ramos aliyejiunga na Madrid kitokea Sevilla mwaka 2005 ameshatwaa mataji yote kwenye mchezo wa soka akianzia ngazi ya klabu hadi kwenye timu ya taifa.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 29 hana furaha kwenye klabu yake hasa kwa kitendo cha klabu hiyo kuamua kumtimua aliyekuwa kocha wao Carlo Ancelotti lakini pia kitendo cha Madrid kushindwa kumpa Euro milioni 10 kwa mwaka kwa ajlili ya kuboresha mkataba mpya.
Ramos aliamini kwamba, angeongezewa mkataba mwingine kwenye majira ya kiangazi ya msimu uliopita baada ya kuifungia timu yake goli la kusawazisha dakika ya mwisho kwenye mchezo wa fainali wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya Atletico Madrid na kuisaidia timu hiyo kunyakua taji hilo kwa mara ya 10 kwenye muda wa nyongeza.
Ramos 3Kwenye mkataba wake wa sasa Ramos anavuna kiasi cha Euro milioni sita kwa mwaka na hajaongezewa kitu kwenye mkataba huo unaomalizika mwaka 2017. Lakini beki huyo wa kati ameshuhudia Rais wa Madrid Florentino Perez akiboresha mikataba ya wachezaji wengine kama Gareth Bale ambaye ameongezewa mshahara wa Euro milioni moja kwa mwaka na sasa atakuwa anavuna kitita cha Euro milioni 10 kwa mwaka kutoka kwenye kile cha milioni tisa kwa mwaka ambazo alikuwa akilipwa mwanzo.
Klabu ya Barcelona imelalamika kuwa, ilipeleka ofa ya kutaka kumsajili Ramos lakini hawakujibiwa chochote na Madrid, kitendo hicho kimemchukiza pia Ramos ambaye amesema anapenda zaidi kukipiga kwenye ligi ya EPL hasa Old Trafford japo bado anawindwa na Barcelona.
Ramos 2

Brazil yatinga robo fainali Neymar akishangilia jukwaani

Neymar mshangiliajiBrazil imepata ushindi wake wa kwanza kwenye mashindano ya Copa America bila ya nyota wake Neymar ambaye usiku wa jana alikuwan jukwaani kama mshangiliaji wakati timu yake inakipiga dhidi ya Venezuela kwenye mchezo wa mwisho wa kundi C ambapo Brazil ilishinda kwa goli 2-1 na kujihakikishia kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Neymar jukwaaniIlibidi Neymar awe jukwaani kuishangilia timu yake kufuatia kulimwa kadi nyekundu na kufungiwa kucheza mechi nne pamoja na faini ya dola 10,000 za kimarekani baada ya kuonesha utovu wa nidhamu kwa kumpiga na mpira mchezaji wa Colombia na kumtolea mwamuzi maneno makali.
Neymar jukwaani 1Thiago Silva aliyenyang’anywa unahodha wa Brazil alianza kuifungia Brazil goli la kwanza zikiwa zimepita dakika tisa tu tangu kuanza kwa mchezo, lakini dakika ya 51 Roberto Firmino akaihakikishia Brazil kufuzu kucheza hatua ya robo fainali baada ya kuifungia timu yake goli la pili akimalizia kazi safi iliyofanywa na Wllian.
Thiago SilvaGoli la kufutia machozi la Venezuela lilifungwa na Miku dakika ya 84 ya  mchezolakini lilikua halina msaada kwa timu yake ambayo imemaliza mkiani kwenye kundi C ikiwa na ponti tatu.
Brazil itakutana na Paraguay kwenye mchezo wake wa robo fainali utakaopigwa siku ya Jumamosi mchezo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkali na wenyekuvutia.
Mchezo mwingine wa kundi C uliopigwa jana usiku ulikuwa  kati ya Colombia dhidi ya Peru, mchezo huo ulimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bila kufungana ambapo Falcao bado ameonekana kushindwa kurejesha makali yake ya kupasia nyavu.

LIVERPOOL YAMFUATA LLORENTE ITALIA

11111111111111111111111
Klabu ya Liverpool ya nchini Uingereza imeamua kumfungia kazi mshambuliaji Fernando Llorente wa Juventus ya Italia katika dirisha hili kubwa la usajili.
Imeelezwa kuwa Liverpool imefikia uamuzi huo baada ya kutokubaliana na dau la mshambuliaji wa Aston Villa, Christian Benteke anayeuzwa kwa dau la paundi 32.5m.
Liverpool imeona dau hilo ni kubwa kwa Benteke na kwamba wameamua kuwafuatilia Fernando Llorente pamoja na mshambuliaji wa mabingwa wa Uropa klabu ya Sevilla ya Hispania, Carlos Bacca.
Ingawa Carlos Bacca ana kipengele kinachomfanya kuuzwa kwa dau lisilopungua paundi 21m lakini Liverpool inaona ni heri zaidi ya dau hilo la Benteke.
Llorente mwenye miaka 30 hivi sasa amekua sio mchezaji muhimu katika kikosi hicho cha mabingwa wa Italia msimu huu na kwamba inaweza kuwa rahisi zaidi kwa Liverpool kumpata kutokana pia Juventus pia wamewasajili Mario Mandzukic pamoja na Dybala huku kijana kutoka Hispania, Morata naye akiwa kikosini.
Inasemekana kuwa kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anahitaji uzoefu katika chumba cha kubadilishia nguo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya vijana wenye umri mdogo.
Tayari Liverpool imewasajili James Milner, Adam Bodgan na Dany Ings huku ikimnasa pia chipukizi anayecheza England U19 Joe Gomez.
Klabu hiyo iko busy kurudi inakostahili baada ya kufanya msimu huu vibaya tofauti na matarajio baada ya kumkosa Luis Suarez waliyemuuza Barcelona pamoja na majeruha ya mara kwa mara ya Daniel Sturridge ambao waliingoza timu hiyo kufanya vizuri misimu miwili iliyopita.
Ikumbukwe kuwa msimu ujao itakua ni mara ya kwanza kwa Liverpool ndani ya karne hii kucheza bila nahodha wao wa muda mrefu, Steven Gerrard anayetimkia Los Angeles Galaxy Marekani.