tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

26 Januari 2016

VAN GAAL UKINGONI, ATIMKIA KWAO, MAZOEZI YAFUTWA, WOODWARD ATETA NA WACHEZAJI WAANDAMIZI, MOURINHO YUPO KIBARAZANI!

MANUNITED-LVG-UKINGONIHABARI NZITO zinavuja huko England kuwa sasa Louis van Gaal yupo ukingoni kuondoka Manchester United huku Mazoezi yaliyopangwa Jumapili na Jumatatu kufutwa na Mtendaji Mkuu, Ed Woodward, akifanya Kikao cha dharura na Wachezaji Waandamizi pamoja na Viongozi wengine wa juu Klabuni hapo.
Habari za ndani zimedai Van Gaal alikutana na Woodward Jumapili na kisha kuruka kwenda kwao Netherlands kuhudhuria kile kilichoitwa Bethdei ya Binti wake wa Kike.
Lakini hali Klabuni hapo ni tete hasa kutokana na presha ya Mashabiki wa Klabu hiyo ambao Jumamosi walimzomea Van Gaal na kumtaka aondoke mara baada ya kufungwa 1-0 na Southampton Uwanjani Old Trafford.
Hicho kilikuwa kipigo chao cha 6 kwenye Ligi Kuu England Msimu huu na kimewatupa Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Leicester City na Pointi 5 nyuma ya Timu ya 4 ambayo ndiyo nafasi ya mwisho ya kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Mbali ya kufungwa, Mashabiki wa Man United hawaridhishwi na staili ya uchezaji ya Van Gaal ambae msisitizo wake ni Difensi.
Huku Van Gaal akitarajiwa mwenyewe kubwaga manyaga badala ya kufukuzwa, zipo kila dalili Jose Mourinho huenda akachukua hatamu hasa baada ya kuvuja habari kuwa Mreno huyo aliandika Barua ya Kurasa 6 kwa Man United akielezea kufaa kwake kuongoza Timu hiyo.
Wakala wa Mourinho, Jorge Mendes, amekanusha kuwepo kwa Barua hiyo na kudai ni upuuzi lakini Waendesha Kamari huko Uingereza wemweka Mourinho kuwa ndie Meneja mpya wa Manchester United.

C1C: LIVERPOOL, EVERTON KUZIMUDU STOKE NA CITY KUTINGA FAINALI KWA DABI YA MERSEYSIDE UWANJANI WEMBLE

C1C: NUSU FAINALI:
Marudiano
**Mechi zote Saa 5 Usiku, Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo katika Meichi ya Kwanza ya Nusu Fainali
Januari 26
-Liverpool v Stoke City [1-0]
Januari 27
-Man City v Everton [1-2]
+++++++++++++++++++++++
CAPITALONECUP-15Liverpool na Everton zinatinga kwenye Mechi za pili za Nusu Fainali ya Kombe la Ligi huko England liitwalo C1C, CAPITAL ONE CUP, huku zikiwa zimeshinda Mechi zao za kwanza.
Liverpool walipata ushindi wa Ugenini wa Bao 1-0 walipoifunga Stoke City huko Britannia Stadium kwaBao la ushindi la Jordon Ibe katika Dakika ya 37 akitokea Benchi kumbadili Philippe Coutinho alieumia Musuli za Pajani.
Kwenye Mechi hii ya pili, Liverpool watakuwa kwao Anfield Jumanne Usiku.
Nao Man City watacheza kwao Etihad Jumatano Usiku wakisaka kupindua kipigo cha 2-1 walichopewa huko Goodison Park katika Mechi ya kwanza.
Katika Mechi hiyo, Everton walitangulia kufunga kwa Bao la Dakika ya 46 la Funer Mori na City kusawazisha kwenye Dakika ya 76 kwa Bao la Jesus Navas.
Lakini Everton walinyakua ushindi kwa Bao la Dakika ya 78 la Romelu Lukaku.
Washindi wa hizi Nusu Fainali watakutana Fainali itakayochezwa hapo Februari 28.
+++++++++++++++++++++++
Nusu Fainali-Kanuni Muhimu:-Kwenye Mechi za Nusu Fainali, ikiwa Jumla ya Magoli kwa Mechi 2 ni sawa baada ya Dakika 90 za Mechi ya Marudiano, Nyongeza ya Dakika 30 itachezwa.
-Ikiwa Gemu ni Sare baada ya hiyo Nyongeza ya Dakika 30, Mshindi atapatikana kwa kuhesabu Goli la Ugenini kuwa mara mbili.
-Ikiwa Gemu bado itakuwa sawa hata baada ya kuhesabu Goli za Ugenini ni mara mbili, basi Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati 5 kama Sheria za Soka zinavyotamka.
+++++++++++++++++++++++

Hakuna maoni: