Kilichoikuta Mallorca msimu wa 1998/99 kwa Van Gaal, kinaweza kuikuta Barcelona msimu huu
Wakati huo ilionekana ni kosa dogo Barca wamefanya na halitokuwa na athari kubwa katika mbio zao za ubingwa.
Hakuna ambaye aliyapa umuhimu mkubwa matokeo ya mechi ile.
Mechi zilizofuatia mbili za Wakatalunya hazikuwa nyepesi, walikuwa wanakutana na Real Madrid CampNou, kisha kufunga safari kwenda Estadio de Anoeta kucheza vs Real Sociedad.
Hata hivyo, kila mtu alitabiri Barca wangewaadhibu vijana wa Zinedine Zidane, na ilikuwa muda wa muafaka kwa Luis Enrique kulipa kisasi dhidi ya Real Sociedad baada ya kufungwa msimu na kidogo aikose kazi yake.
Haikuwa rahisi kama ilivyoadhaniwa, Barca wakapoteza mechi zote mbili na tangu hapo mambo yakazidi kuharibika.
Wakati Valencia walipoenda Camp Nou miezi miwili iliyopita, Barcelona waliwafunga magoli 7 katika nusu fainali ya Copa del Rey na kuelekea mchezo wa jana jumapili Barca walipewa nafasi ya kuweza kurejea katika kiwango chao.
Barca walionekana kuimarika katika mchezo wa jana, lakini walikuwa ni Valencia waliorudi kwenye ubora wao ambao walihakikishia Barcelona anaangukia pua kwene mchezo wa 3 mfululizo wa ligi, mara ya kwanza tangu mwaka 2003.
Huku kukiwa kumebakiwa mechi 5 kabla ya msimu kumalizika – kwa hakika Barcelona hawatotaka kupata matokeo mabaya tena, wanaweza kujikuta wamegeuka Real Mallorca ya msimu wa 1998/99 na Atletico au Real Madrid wakawa Barca ya msimu huo, kwa kutwaa La Liga baada ya kuachwa nyuma kwa pointi nyingi na viongozi wa ligi kabla ya kuwafikia na kuwazidi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni