WENGER AKATA TAMAA UBINGWA AHIMIZA VITA KUBAKI 4 BORA!
Matokeo ya Jana yamewaacha Arsenal wakiwa Nafasi ya 4 kwenye BPL
wakiwa nyuma ya Timu ya 3 Man City kwa tofauti ya Magoli na wakiwa
Pointi 13 nyuma ya Vinara Leicester City huku wao wakibakisha Mechi 5.
Nyuma ya Arsenal zipo Man United na West Ham ambazo nazo zina
matumaini ya kuingia 4 Bora na kuinyima Timu ya Wenger kumaliza ndani ya
4 Bora kwa mara ya 20 mfululizo.
Baada ya Mechi hiyo na Palace, Wenger aliongea: "Ukweli baada ya
Gemu ya Lei sipo kwenye hali njema kuongelea kutwaa Ubingwa. Nipo kwenye
hali ya kuitengeneza Timu kiakili kwa ajili ya Mechi ijayo Alhamisi na
West Brom. Ni muhimu kuzitazama Timu za nyuma yetu kwani zinacheza
vizuri na zinashinda!"
Aliongeza: "Kwetu tunapaswa kupigana hadi mwisho ili tuwemo 4 Bora!"
LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
Jumatatu Aprili 18
2200 Stoke v Tottenham
Jumanne Aprili 19
2145 Newcastle v Man City
Jumatano Aprili 20
2145 West Ham v Watford
2200 Liverpool v Everton
2200 Man United v Crystal Palace
Alhamisi Aprili 21
2145 Arsenal v West Brom
Jumamosi Aprili 23
1445 Man City v Stoke
1700 Aston Villa v Southampton
1700 Bournemouth v Chelsea
1700 Liverpool v Newcastle
Jumapili Aprili 24
1605 Sunderland v Arsenal
1815 Leicester v Swansea
Jumatatu Aprili 25
2200 Tottenham v West Brom
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni