PELLEGRINI, BENITEZ, NDANI YA MAKOCHA WANNE WANAOPEWA NAFASI EVERTON
Jana Roberto MartÃnez alifukuzwa kunako klabu ya Everton baada ya
kudumu kwa misimu mitatu. Sasa swali kubwa lililobaki je, ni nani wa
kurithi mikoba yake?. Hii ni orodha ya makocha wanne wanaopewa nafasi
kubwa ya kuchukua mikoba yake Everton.
- Frank de Boer
Legend huyu wa Ajax amekuwa akihusishwa sana na kujiunga na
Everton. Tayari ameshajiuzulu kufundisha Ajax. Hatua hii hii inaongeza
ukweli wa Mdachi huyo kujiunga na ‘Toffees’. Huku akiwa ameipa Ajax
mataji ya manne mfululizo ya Ligi ya Uholanzi maarufu kama Eredivise,
rekodi hiyo inampa nafasi kubwa ya kubeba mikoba ya Martinez kunako
klabu ya Everton.
- David Moyes
Moyes ambaye ni raia wa Scotland aliwahi pia kuifundisha klabu hiyo
na kudumu kwa miaka 11 kabla ya kuelekea kunako klabu ya Manchester
United na Real Sociedad. Licha ya kwamba alishindwa kuonesha makali yake
kwenye vilabu hivyo, Moyes ni kocha mzuri na mwenye mahusiano mazuri na
klabu hiyo. Pia anapewa nafasi kubwa ya kurudi ili kuja kurejesha
heshima ya klabu.
3. Manuel Pellegrini
Kocha huyu raia wa Chile amejijengea heshima kubwa sana kunako ligi
ya England licha ya kibarua chake na Manchester City kuisha mwishoni mwa
msimu huu na kutoongezewa muda mwingine na nafasi yake kuchukuliwa na
Mhispaniola Pep Guardiola ambaye ataanza rasmi kazi mwezi July.
Akiwa na klabu ya Manchester City, Pellegrini amefanikiwa kuleta makombe kadhaa ikiwemo la ligi kuu.
Akiwa na klabu ya Manchester City, Pellegrini amefanikiwa kuleta makombe kadhaa ikiwemo la ligi kuu.
4. Rafa Benitez
Mashabiki wa Everton pengine wanaweza wasiwe na mapenzi ama imani
naye kutokana na kufundisha Liverpool siku za nyuma – ambao ni mahasimu
wakubwa wa Liverpool
Lakini uwezo wa mkufunzi huyo raia wa Uhispania si wa kutilia mashaka
kutokana na rekodi aliyoweka katika siku za nyuma. Moja ya rekodi zake
kubwa ni pamoja na kuchukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na
Liverpool mwaka 2005 na vile vile kufundisha timu vigogo kama vile Inter
Milan na Real Madrid. Kwa ufupi Benitez ni moja ya makocha
watakaoisaidi kwa kiasi kikubwa Everton.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni