Wiki 1 baada ya Patrick Ekeng kufariki, Mcameroon mwingine adondoka uwanjani na kufariki
Golikipa wa timu ya taifa ya wanawake ya Cameroon amefariki dunia baada ya kuanguka ghafla wakati akipasha misuli, shirikisho la soka la Cameroon limesema.
Jeanine Christelle Djomnang, 26, alianza kujisikia vibaya kabla ya mechi ya Femina Stars Ebolowa kusini mwa Cameroon jumapili iliyopita, na akafariki njiani akiwa anapelekwa hospitali.
Taarifa ya shirikisho ya mwanzo inaripoti kwamba mwanadada huyo alifariki kutokana na mshtuko wa moyo lakini bado taarifa rasmi ya kitabibu haijatoka.
Kifo cha golikipa huyu kinakuja siku chache baada ya mwanasoka wa nchi hiyo Patrick Ekeng kufariki uwanjani nchini Romania.
Djomnang alilamika kuwa na maumivu ya kifua wakati akijiandaa kucheza dhidi ya Louves MINPROFF Yaounde katika ligi ya wanawake ya Cameroon na muda mfupi akiwa anapasha misuli akadondoka na kupelekwa hospital.
Mwanasoka bora wa Cameroon wa mwaka upande wa Wanawake Gaelle Enganamouit, ambaye kwa sasa anacheza soka nchinu Sweden, alikuwa mmoja ya wachezaji waliosikitishwa na taarifa hizo.
Ijumaa iliyopita ilithibitishwa kwamba mchezaji wa Dinamo Bucharest na mcameroon Patrick Ekeng alifariki dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo na kuanguka uwanjani.
Kiungo huyo aliyekuwa na miaka 26 alianguka dakika 70 ya mchezo uliokuwa ukionyeshwa live baina ya Dinamo Vs Viitorul. Alifariki baadae hosptali.
Kitabu cha maombelezo kimefunguliwa katika makuu ya shirikisho la soka la Cameroon kwa ajili ya Ekeng na Djomanang.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni