tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

12 Agosti 2016

LIGI KUU ENGLAND KUANZA WIKIENDI, WACHAMBUZI WATABIRI!


PATA UNDANI!
BPL-2016-17LIGI KUU ENGLAND inaanza Wikiendi hii na Duniani kote Wachambuzi na Mashabiki wametumbukia kwenye Mdahalo, hasa mabishano, ya nini kitajiri.
Lakini wengi, kama si wote, wameafiki kitu kimoja tu.
Leicester City, Mabingwa wa England, hawana nafasi hata chembe kutetea Taji lao na kama hawashuki Daraja basi wataelea katikati ya msimamo wa Ligi.
Baadhi ya Wachambuzi ambao tutawanukuu hapa ni wale wa Sky Sports ya England ambao ni Wachezaji wa zamani na ni Gary Neville [Manchester United], Jamie Carragher [Liverpool], Thierry Henry [Arsenal], Graeme Souness [Liverpool]na Jamie Redknapp [Liverpool, Tottenham, Southampton].
NINI WAMESEMA NA BINGWA NANI:
-GARY NEVILLE: Man United
-Wana Meneja Mpya Jose Mourinho na Wachezaji wapya lakini wawili ndio hatari Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba na sasa jeuri yao imerudi.
here are players wearing that shirt who will stick their chests out - and that's what Manchester United are all about.
-4 BORA: 1. Man Utd 2. Arsenal 3. Man City 4. Liverpool
-Mabingwa Leicester: Kumaliza Nafasi ya 7 hadi 10
-Mfungaji Bora: Sergio Aguero        
-Mchezaji wa Mvuto: Zlatan Ibrahimovic
CARRAGHER: Man City
Chini ya Pep Guardiola watakuwa na njaa ya Ubingwa na wapo Nyota wazuri David Silva, Sergio Aguero na Kevin De Bruyne.
-4 BORA: Man City 2. Chelsea 3. Man United 4. Liverpool
-Mabingwa Leicester: Kati ya Msimamo wa Ligi
-Mfungaji Bora: Harry Kane   
-Mchezaji wa Mvuto: Kevin De Bruyne
HENRY: Man City
Matumaini yangu ni kwa Arsenal.
Lakini nadhani Bingwa ni kati ya Man City na Man United.
Guardiola ameshinda kila sehemu aliyotua na Wachezaji wakimuelewa watatwaa Ubingwa.
-4 BORA: 1. Man City 2. Man Utd. 3. Chelsea 4. Arsenal
-Mabingwa Leicester: Katikati ya Msimamo
-Mfungaji Bora: Sergio Aguero        
-Mchezaji wa Mvuto: Sadio Mane
REDKNAPP: Man City
Bila ya Vincent Kompany na Sergio Aguero kuwa fiti Ubingwa kwao ni shida..
-4 BORA: 1. Man City 2. Man Utd 3. Tottenham 4. Liverpool
-Mabingwa Leicester: 6 Bora
-Mfungaji Bora: Harry Kane   
-Mchezaji wa Mvuto: De Bruyne
SOUNESS: Man United
Bingwa ni Klabu ya Jiji la Manchester na kama Ibrahimovic atawika basi ni Man united.
-4 BORA: 1. Man Utd 2. Man City. 3. Tottenham 4. Arsenal
-Mabingwa Leicester: Nafasi ya 4 hadi 8
-Mfungaji Bora: Sergio Aguero   

Hakuna maoni: