WAWILI WAHAMA MAN UNITED, STRAIKA ARGENTINA YUPO WEST HAM, SWANSEA YAWEKA REKODI KWA STRAIKA WA ATLETI!
Sunderland yawasaini Mabeki Wawili wa Manchester United Paddy McNair na Donald Love kwa Dau la Jumla la Pauni Milioni 5.5.
Chipukizi hao wote wenye Miaka 21 wamesaini Mkataba wa Miaka Minne kila mmoja chini ya Meneja Mpya wa Sunderland, David Moyes, ambae alitimuliwa Man United Miaka Miwili iliyopita baada ya kudumu Miezi 10 tu.
McNair, ambae aliwakilisha Nchi yake Northern Ireland huko Euro 2016, aliichezea Timu ya Kwanza ya Man United kwa mara ya kwanza Septemba 2014 na kucheza Jumla ya Mechi 27.
Love, ambae ni Raia wa Scotland, alikuwa kwa Mkopo huko Wigan Msimu uliopita na amewahi kuichezea Timu ya Kwanza ya Man United mara 2.
WEST HAM YAMSAINI STRAIKA WA ARGENTINA
Calleri, mwenye Miaka 22, aliwakilisha Argentina huko Brazil kwenye Michezo ya Olimpiki ambako Jumatano Usiku ilitupwa nje baada ya kushindwa kuvuka Kundi lao.
Calleri alikuwa huko Brazil kwa Mkopo kwenye Klabu ya Sao Paolo na kuwa Mfungaji Bora kwenye Copa Libertadores.
West Ham, chini ya Meneja Slaven Bilic, itafungua dimba Msimu wao mpya wa Ligi Kuu England Jumatatu Usiku kwa kucheza Ugenini huko Stamford Bridge na Chelsea.
SWANSEA YAWEKA REKODI KWA STRAIKA WA ATLETI!
Swansea City wamevunja Rekodi ya Klabu yao kwa kumsaini Straika kutoka Spain Borja Baston kutoka Atletico Madrid kwa Pauni Milioni 15.
Borja, mwenye Miaka 23, alifunga Bao 18 kwenye La Liga Msimu uliopita akiwa kwa Mkopo na Eibar.
Dau la kumnunua Borja limiezidi lile la Mwaka 2013 Swansea walipomnunua Wilfried Bony.
Borja amekuja wakati muafaka baada ya Swansea kuondokewa na Mafowadi Andre Ayew alieenda West Ham, Alberto Paloschi, Eder na Bafetimbi Gomis.
Hivi Juzi Swansea pia walimchukua Mchezaji mwingine wa Spain Fernando Llorente na hadi sasa Kocha Mpya Francesco Guidolin ameshasaini Wachezaji Watano na wengine ni Beki wa Holland Mike van der Hoorn, Winga wa Holland Leroy Fer na Kipa wa Australian Mark Birighitti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni