Sanchez ahusishwa na Juventus
Gazeti maarufu la michezo nchini Italia la Tutto Sport limeandika kuhusu mpango wa Juventus kwa Sanchez.Katika mpango huo wa Juventus wanataka kufanya usajili huo kwa kuwapa Miralem Pjanic.
Sanchez ambae mkataba wake umebakiza miezi michache
kuisha amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Arsenal.Tetesi za yeye
kuondoka Gunnerz zinazidi kusambaa baada ya Sanchez kugoma kusaini
mkataba mpya wa kukipiga Guners hadi hapo watakapomuongezea mkataba.
Timu nyingi ikiwemo PSG pamoja na timu za China zimekuwa
zikipigana vikumbo kuhusiana na saini ya mchezaji huyo.Lakini sasa
Juventus nao wameingia kwenye mbio hizo.Taarifa zilizotolewa na gazeti
la Tuttos zinasema Juventus wanataka kumuweka Miralem Pjanic kuwa sehemu
ya dili hilo.
Sanchez anaonekana uhusiano wake na Wenger unazidi
kuporomoka kwani wikiendi hii alionekana mwenye hasira kubwa bada ya
kutolewa katika mchezo zidi ya Swansea.Sanchez anataka Arsenal
wamuongezee mkataba awe analipwa £280,000 kwa wiki jambo ambalo
linaonekana gumu.
Juventus baada ya kufanya usajili wa rekodi Italia kwa
kumchukua Higuain kwa dau la £76m akitokea Napoli.Baada ya kumuuza Paul
Pogba Juventus wanaonekana kuxidi kutaka kuitengeneza timu yao na
kumtafuta mtu wa kucheza pamoja na Paulo Dyabala na Gonzalo
Higuain,Sanchez anaonekana mtu sahihi kwao kwa sasa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni