MTU 20 MAN UNITED WAPAA URUSI KUIVAA FC ROSTOV!
MASHABIKI WAO WAONYWA KUTOVAA JEZI ZA TIMU YAO HUKO RUSSIA!!
Man
United itaivaa FC Rostov Alhamisi Usiku huko Mjini Rostov Nchini Russia
kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA
LIGI.
Ili
kukwepa vurugu kama zile zilizotokea huko France Mwezi Juni wakati wa
Fainali za EURO 2016 wakati Mashabiki wa Russia walipowashambulia wale
wa England, Mashabiki wa Man United wameshauriwa kutovaa Jezi za Klabu
hiyo wakiwa matembezini Mjini Rostov.
Mkuu
wa Kitengo cha Tiketi na Uanachama cha Man United, Sam Kelleher,
amewaandikia Mashabiki wote wanaosafiri kwenda Rostov kuwapa ushauri wa
kujilinda wakiwa huko Russia.
Mbali
ya kushauriwa kutovaa Jezi za Man United wakiwa matembezini Mjini
Rostov, pia wametakiwa kutotembea mmoja mmoja bali wawe kwenye vikundi.
WAKATI HUO HUO, Meneja Jose Mourinho ameteua Wachezaki 20 walioruka Jioni hii kwenda huko Urusi na Kepteni Wayne Rooney hayumo Kikosini.
Pia
Luke Shaw na Bastian Schweinsteiger hawamo kwenye Kikosi hicho pamoja
na Eric Bailly ambae yuko Kifungoni Mechi 1 baada ya kutolewa nje kwa
Kadi Nyekundu katika Mechi iliyopita dhidi ya Saint-Etienne.
Habari
njema kwa Man United ni kupona kwa Henrikh Mkhitaryan ambae aliumia
kwenye Mechi na Saint-Etienne na kuzikosa Mechi 2 zilizopita zile za
Fainali ya EFL CUP Man United ilipoifunga Southampton na kutwaa Kombe na
ile Sare ya Juzi na Bournemouth.
KIKOSI KAMILI KILICHOSAFIRI:
De
Gea, Romero, O'Hara; Valencia, Jones, Rojo, Smalling, Blind, Darmian,
Young; Carrick, Herrera, Fellaini, Pogba, Mata, Lingard, Mkhitaryan;
Martial, Rashford, Ibrahimovic.
UEFA EUROPA LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Mechi za Kwanza [Marudiano Machi 16]
**Saa za Bongo
2100 Apoel Nicosia (Cyprus) v Anderlecht (Belgium)
2100 FC Rostov (Russia) v Manchester United (England)
2100 FC Copenhagen (Denmark) v Ajax (Netherland)
2305 Celta Vigo (Spain) v FC Krasnodar (Russia)
2305 Schalke (Germany) v Borussia Monchengladbach (Germany)
2305 Lyon (France) v Roma (Italy)
2305 Olympiakos (Greece) v Besiktas (Turkey)
2305 KAA Gent (Belgium) v KRC Genk (Belgium)
+++++++++++++++++++++++++++++
UEFA EUROPA LIGITarehe Muhimu:
09/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi za Kwanza
16/03/17: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Marudiano
13/04/17: Robo Fainali, Mechi za Kwanza
20/04/17: Robo Fainali, Mechi za Pili
04/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
11/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
FAINALI
24 Mei 2017: Friends Arena, Solna, Sweden
KISAGO CHA BAO 10: WENGER ‘ACHEFULIWA’ NA REFA!
Jana Refa kutoka Greece Anastasios Sidiropoulos aliwapa Penati Bayern wakati Arsenal ikiongoza 1-0 na hapo hapo kumtoa nje kwa Kadi Nyekundu Sentahafu Laurent Koscielny na Bayern kusawazisha kwa Penati hiyo na kisha kushindilia Bao nyingine 4 na kushinda 5-1.
Katika Mechi ya Kwanza huko Germany Arsenal pia ilipigwa 5-1 na Bayern na hivyo kutupwa nje ya Hatua ya Mtoano ya Timu 16 kwa Jumla ya Bao 10-2.
Hii ni mara ya 7 mfululizo kwa Arsenal kushindwa kuivuka Hatuai hii ya UCL.
Wenger ameeleza: “Penati na Kadi Nyekundu havielezeki na ni kashfa. Ni uchezeshaji ovyo wa Refa. Nimekasirika na kuhuzunika sana!”
Vile vile Wenger alidai Refa huyo Mgiriki aliwanyima Penati katika Kipindi cha Kwanza wakati Xabi Alonso alipomchezea Faulo Theo Walcott huku pia akidai Straika wa Bayern Lewandowski alikuwa Ofsaidi katika muvu ambayo Koscielny alimchezea Rafu Straika huyo na kuzaa Penati na Kadi Nyekundu.
Wenger pia alishangazwa na kitendo cha Refa huyo kwanza kumpa Kadi ya Njano Koscielny na kisha kuibadili kuwa Kadi Nyekundu baada ya ushauri wa Refa Msaidizi aliekuwa nyuma ya Goli.
Mbali ya janga na aibu ya kushushiwa kipigo kitakatifu, kabla ya Mechi hiyo kuanza Wenger pia alikumbana na adha ya Mashabiki wa Arsenal waliomtaka ajiuzulu na kuinua Mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kumtaka ang’oke.
Alipohojiwa kuhusu Washabiki hao, Wenger alijibu hana la kusema.
UEFA CHAMPIONZ LIGI: LEO BARCA KUIRUDIA PSG ILIYOWABAMIZA 4, KOCHA LUIS ENRIQUE ADAI BARCA INAWEZA KUPIGA 6!
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 - Mechi za Pili
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
Jumatano 8 Machi 2017
Barcelona v Paris Saint Germain [0-4]
Borussia Dortmund v Benfica [0-1]
+++++++++++++++++++++++++
Wiki 3 zilizopita, PSG iliinyuka Barca 4-0 huko Paris katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI na Leo Barca wanahitaji Bao 4-0 kusonga Robo Fainali au ushindi wowote wenye tofauti ya Bao 4-0 kwa upande wao.
Akiongea Jana Jumanne, Enrique amesema: “Ikiwa wao wameweza kutufunga 4, sisi tunaweza kufunga 6!”
Aliongeza: “Hatuna cha kupoteza na mengi ya kushinda!”
Mara baada ya kipigo hicho cha PSG, Barcelona wakarejea Spain kwenye La Liga na kuzitandika Sporting Gijon 6-1 na Celta Vigo 5-0.
Msimu huu, wakiwa kwao Nou Camp, Barcelona imeshatoa vipondo vizito kwenye UCL kwa kuzichapa Celtic 7-0, Manchester City 4-0 na Borussia Moenchengladbach 4-0.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 - Mechi za Pili
Matokeo”
**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi 2
Jumanne 7 Machi 2017
Arsenal 1 Bayern Munich 5 [2-10]
Napoli 1 Real Madrid 3 [2-6]
+++++++++++++++++++++++++
Ratiba:
Mechi za Pili
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
Jumanne 14 Machi 2017
Juventus v FC Porto [2-0]
Leicester City v Sevilla [1-2]
Jumatano 15 Machi 2017
Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen [4-2]
Monaco v Manchester City [3-5]
++++++++++++++++++++++++++++
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MTOANO:
14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza
7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
UEFA CHAMPIONZ LIGI: MABINGWA REAL WAIPIGA TENA 3 NAPOLI!
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 - Mechi za Pili
**Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi 2
Jumanne 7 Machi 2017
Arsenal 1 Bayern Munich 5 [2-10]
Napoli 1 Real Madrid 3 [2-6]
+++++++++++++++++++++++++
Dakika ya 24 Napoli walienda 1-0 mbele kwa Bao la Dries Mertens.
Bao hilo lilidumu hadi Mapumziko.
Dakika ya 52 Kona ya Toni Kroos ilifungwa kwa Kichwa na Sergio Ramos na Gemu kuwa 1-1.
Dakika ya 57 Kona nyingine ya Kroos ilimaliziwa na Ramos na Real kuandika Bao la Pili.
Real walipiga Bao lao la 3 Dakika ya 90 baada ya Shuti la Cristiano Ronaldo kuokolewa na Kipa Reina na Alvaro Morata, alietokea Benchi, kuukwamisha Mpira huo uliotemwa.
Hadi mwisho Napoli 1 Real 3.
VIKOSI:
NAPOLI: Pepe Reina, Alexander Soderlund, Raul Albiol, Kalidou Koulibaly, Faouzi Ghoulam, Allan, Amadou Diawara, Marek Hamsik, Jose Callejon, Dries Mertens, Lorenzo Insigne
Akiba: Rafael Cabral Barbosa, Jorginho, Christian Maggio, Nikola Maksimovic, Piotr Zielinski, Marko Rog, Arkadiusz Milik
REAL MADRID: Keylor Navas, Dani Carvajal, Pepe, Sergio Ramos, Marcelo, Toni Kroos, Casemiro, Luka Modric, Gareth Bale, Karim Benzema, Cristiano Ronaldo
Akiba: Nacho, James Rodriguez, Kiko Casilla, Lucas, Alvaro Morata, Isco, Danilo
REFA: Cuneyt Cakir [Turkey]
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Mechi za Pili
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
Jumatano 8 Machi 2017
Barcelona v Paris Saint Germain [0-4]
Borussia Dortmund v Benfica [0-1]
Jumanne 14 Machi 2017
Juventus v FC Porto [2-0]
Leicester City v Sevilla [1-2]
Jumatano 15 Machi 2017
Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen [4-2]
Monaco v Manchester City [3-5]
++++++++++++++++++++++++++++
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MTOANO:
14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza
7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni