tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

17 Mei 2017

2 ZA 4 BORA KATI YA CITY, LIVERPOOL NA ARSENAL KUAMULIWA SIKU YA MWISHO JUMAPILI!
EPL-SOKATAMU-SIT-1WAKATI Mabingwa wapya Chelsea na Tottenham Hotspur tayari zishakata Tiketi 2 za Timu 4 Bora za EPL, LIGI KUU ENGLAND, vita imebaki 2 zipi za mwisho zitaungana nao.
 
Vita hiyo sasa imebaki kwa Liverpool, Man City na Arsenal ambayo itaamuliwa kwenye Mechi za mwisho za Msimu hapo Jumapili Mei 21 baada Jana Man City na Arsenal zote kushinda Mechi zao za Kiporo.
 
Jana Man City wakiwa kwao Etihad waliitandika West Bromwich Albion 3-1 huku Bao zao zikipigwa na Gabriel Jesus, Dakika ya 27, Kevin De Bruyne, 29, na Yaya Toure, 57.
Bao la WBA lilifungwa na Robson-Kanu Dakika ya 87.
 
Kwenye Mechi yao ya mwisho hapo Jumapili Ugenini na Watford, Man City wanahitaji Sare tu ili kujihakikishia kuwemo 4 Bora.
 
Huko Emirates Jijini London, Arsenal waliifunga Timu ambayo tayari ilishashushwa Daraja Sunderland Bao 2-0 zote zikifungwa Kipindi cha Pili na Alexis Sanchez na kujiwekea matumaini ya kufuzu 4 Bora ikiwa mambo kadhaa yatatokea hapo Jumapili kwenye Mechi za mwisho kabisa za Ligi.

Hapo Jumapili Arsenal kwanza inapaswa kuifunga Timu ya 7 Everton na pia kuomba Liverpool inafungwa na Middlesbrough ambayo tayari ishashuka Daraja.
Arsenal wapo Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 1 nyuma ya Liverpool ambao pia wana Goli 2 zaidi katika Tofauti ya Magoli.
 
ARSENAL KUMALIZA 4 BORA - LAZIMA:
-Washinde na Liverpool ishindwe kuifunga Boro.
-Watoke Sare 0-0 au 1-1 na Liverpool kwa Bao 3 au zaidi.
-Wapate Sare ya Magoli ya 2-2 na Liverpool wafungwe 2-0 au Sare 3-3 na Liverpool wafungwe 3-1 na kadhalika.
-Washinde na Man City wafungwe na kubadili tofauti ya Magoli.na kuwa zaidi ya 5.

 
LIVERPOOL WATAMALIZA 4 BORA IKIWA:
-Watashinda au watapata matokeo yeyote bora kupita Arsenal
EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba/Matokeo:
Jumatatu Mei 15
Chelsea 4 Watford 3             
Jumanne Mei 16
Arsenal 2 Sunderland 0         
Manchester City 3 West Bromwich Albion 1
Jumatano Mei 17
2145 Southampton v Manchester United         
Alhamisi Mei 18
2145 Leicester City v Tottenham Hotspur         
Jumapili Mei 21
Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni
Arsenal v Everton            
Burnley v West Ham United                 
Chelsea v Sunderland                 
Hull City v Tottenham Hotspur              
Leicester City v Bournemouth               
Liverpool v Middlesbrough          
Manchester United v Crystal Palace                 
Southampton v Stoke City          
Swansea City v West Bromwich Albion            
Watford v Manchester City

Hakuna maoni: