Mino Raiola ajisafisha kuhusu Pogba huku Mourinho akiwatuliza mashabiki
Raiola imebainika katika usajili wa Pogba alikula kiasi cha £41m kiasi ambacho kinaonekana ni kikubwa sana kiasi cha FIFA kutilia mashaka dili hilo.
Raiola ameibuka na kukanusha vikali kwamba kulikuwa na mchezo haramu wakati Pogba akisajiliwa United na kusisitiza kila kitu kilikuwa sawa na £41m ilikuwa halali kabisa.
“Sikupewa hela ya ziada na upande wowote sio Juve wala United, kila nilichopata kilikuwepo ndani ya mkataba” alisema Riola na kusisitiza kwamba pesa anazodaiwa kupewa kimagumashi hazipo.
Raiola amesema yeye hukaa na wateja wake na kuwaambia wazi kwamba watakwenda wanapoona wanahitajika na United walimuhitaji Pogba ndio maana akaenda United.
Raiola amedai taarifa hizo zinamshangaza kwani Paul Pogba kurudi United ni kama mtoto aliyerudi nyumbani na hata haikuwa na haja ya nguvu ya ziada kutumika katika usajili huo.
Raiola amesema United ni klabu ambayo inaweza kufanya lolote wanalotaka katika usajili tofauti na Arsenal na ndio maana sio ngumu kwao kumnunua mchezaji yeyote.
Wakati Raiola akijitahidi kujisafisha kuhusu Pogba, kocha wa Manchester United Jose Mourinho amewaambia mashabiki wa United wasiwe na shaka kuhusu Pogba.
“Suala rahisi sana kwani ukweli ni kwamba haliwezi kumuathiri Pogba” alisema Mourinho na Pogba mwenyewe alionekana akiwa uwanja wa United wa mazoezi kama kawaida akichukua mazoezi na timu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni