tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

13 Mei 2017

POGBA AFIWA NA BABA MZAZI!


POGBA-BABABABA Mzazi wa Kiungo wa Manchester United Paul Pogba amefariki Dunia akiwa na Miaka 79 baada ya kuugua.
Fassou Antoine Pogba aliihama Nchi yake Guinea kutoka Afrika na kwenda Paris, France akiwa na Miaka 30.
Mbali ya Paul Pogba, Watoto wake wengine ni Mapacha Florentin na Mathias ambao wote ni Wanasoka.
Wakati Pogba akiamua kuichezea France, Ndugu zake Florentin na Mathias wao waliamua kuiwakilisha Guinea.POGBA-BETHDEI
Familia ya Pogba ilithibitisha kwa Gazeti la France, Le Parisien, kuwa Mzee Fassou Antoine Pogba, aliekuwa akiugua, alifariki Jana Ijumaa.
Mwaka Jana kwenye Fainali za EURO 2016, Mzee Fassou alionekana Jukwaani Uwanjani akiwa na Wanawe Florentin na Mathias wakimshangilia Paul Pogba akiichezea France walipokutana na Switzerland.
Mwezi Machi Pogba alitoa Picha kwenye Instagram akisheherekea Siku ya Kuzaliwa ya Baba yake na kuandika: 'Happy birthday dear Dad, I feel blessed to be your son #pogdaddy #fighter #pogbance.'
Mzee Fassou alitua France akiwa hana hata Senti Moja lakini hakusahau Soka lake aliloanzia huko kwao Guinea na baadae kuendelea kuwa Kocha akiwafundisha pia Wanawe Watatu huko Roissy-en-Brie.
Mwaka 2016 alipohojiwa na Wanahabari alinena: “Nilicheza Soka Madaraja ya chini kupita nilivyotaka. Nilitaka Wanangu wacheze Madaraja ya juu, Nilikuwa mkali mno kwao walipokuwa wadogo na hilo liliwafanya wajifunze haraka. Ilifika wakati nafundisha Watoto wengine ili mradi Paul aweze kucheza akiwa na Miaka Minne, Mitano, Sita. Nilitaka wawe kiwango cha juu kabisa!”
LALA KWA AMANI, Baba yetu.

Hakuna maoni: