tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

1 Mei 2017

Sulley Muntari akumbana na ubaguzi wa rangi, aamua kutoka uwanjani.


Kati ya ligi zinazoonekana vitendo vya kibaguzi kutawala ni ligi kuu nchini Italia almaarufu kama Serie A, wachezaji wengi sana Wakiafrika wamekuwa wakikutana na vitendo hivi ambavyo sio vya kiungwana.
Wikiendi hii ilikuwa zamu ya kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Ghana pamoja na klabu ya Ac Millan ambaye sasa anaichezea klabu ya Pescara Sulley Muntari ambaye alikutana na mashabiki wakorofi wabaguzi wa rangi.
Muntari anadai mashabiki wa klabu ya Cagliari ni kama walimpania kwani tangu mchezo unaanza dakika ya kwanza walikuwa wakimzomea sana kila anapokimbilia mpira huku wakiimba nyimbo za kuhusu ngozi yake.
Mbaya zaidi kwa Muntari anasema kulikuwa na kundi la watoto wadogo kabisa ambao nao walikuwa na wazazi wao lakini cha ajabu watoto wale nao walikuwa wakimzomea Muntari kutokana na rangi yake.
“Wakati kipindi cha kwanza tunacheza niliona kundi la watoto wakiwa na wazazi wao wakiwa wananizomea sana, niliamua kuwafuata na kuwapa jezi yangu kama mfano wakatulia” alisema Muntari.
Muntari anadai wakati wanarudi tena uwanjani kipindi cha pili kulijitokeza kundi lingine ambao wao sasa walikuwa wakizomea zaidi na kumuimba zaidi, kitendo ambacho kilimkera na kumuumiza sana.
“Wakati hili kundi lingine likinizomea nilijaribu kumfuata muamuzi kumuambia kuhusu kelele hizo, cha ajabu aliniambia endelea kucheza mpira badala ya kutuliza hali ya mashabiki, hapo nilikasirika sana na nikaamua kuondoka”, Muntari alitoka dakika tank kabla ya mchezo huo kuisha na kuifanya timu yake kumaliza 10 uwanjani.
Muntari amesisitiza kwa kuwaambia wazungu kwamba “hii ni rangi yangu na najivunia” huku kocha wake Zdenek Zeman akimtupia lawama muamuzi wa pambano hilo kwa kushindwa kutafuta namna ya kuwatuliza mashabiki.
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Juventus Alessandro Del Piero amemkingia kifua Muntari kwa kusema kwamba wakati mwingine ni vyema kufanya mambo ili kuwa onyo kwa mashabiki na waamuzi.

Hakuna maoni: