WENGER AUNGAMA, MAHASIMU WAO SPURS NI MOTO!
JUMAPILI ARSENAL KUWAVAA MAN UNITED!
Kipigo
hicho kimehakikisha Kikosi cha Spurs chini ya Meneja Mauricio
Pochettino sasa kitamaliza kikiwa juu ya Arsenal kwenye Msimamo wa Ligi
kwa mara ya kwanza katika Miaka 22.
Baada
Mechi 34 Spurs wako.Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 77 na Arsenal wapo
Nafasi ya 6 wakiwa wamecheza Mechi 33 na wana Pointi 60.
Wenger ameeleza: "Tazama, Pointi ni Pointi.
Hazitoki mbinguni unazipata Uwanjani.
Nkiamini au nisiamini pengo lipo!"
Katika Miaka yake zaidi ya 20 akiwa na Arsenal, Wenger hajawahi kumaliza nje ya 4 Bora ya Ligi lakini safari hii yupo hatarini kulikosa hilo huku faraja pekee kwao ni kutinga Nusu Fainali ya FA CUP ambayo watacheza na Chelsea.
Katika Miaka yake zaidi ya 20 akiwa na Arsenal, Wenger hajawahi kumaliza nje ya 4 Bora ya Ligi lakini safari hii yupo hatarini kulikosa hilo huku faraja pekee kwao ni kutinga Nusu Fainali ya FA CUP ambayo watacheza na Chelsea.
Jumapili Arsenal wataikaribisha Emirates Man United iliyo Nafasi ya 5 na ambao wako Pointi 5 mbele yao huku Man City ambao wako Nafasi ya 4 wako Pointi 6 mbele ya Arsenal.
Wenger amesema: "Ni ngumu sasa lakini ni lazima tupigane! Bado tuna nafasi 4 Bora inabidi tujikokote toka hapa na kujitayarisha kwa Gemu zetu zijazo!"
EPL, LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
Jumatatu Mei 1
2200 Watford v Liverpool
Ijumaa Mei 5
2200 West Ham United V Tottenham Hotspur
Jumamosi Mei 6
1430 Manchester City V Crystal Palace
1700 Bournemouth V Stoke City
1700 Burnley V West Bromwich Albion
1700 Hull City V Sunderland
1700 Leicester City V Watford
1930 Swansea City V Everton
Jumapili Mei 7
1530 Liverpool V Southampton
1800 Arsenal V Manchester United
Jumatatu Mei 8
2200 Chelsea V Middlesbrough
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni