tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

13 Oktoba 2017

Lukaku anaweza kuweka rekodi hii? Koeman atatimuliwa? Haya ni baadhi ya maswali ya kujiuliza kuelekea weekend ya Epl


Michezo ya kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa wiki hii imemalizika na sasa tunakwenda katika ligi za vilabu, na kati ya wiki tamu katika soka ni wiki hii kwani mitanange mingi itakuwa moto moto.
Klopp atafanyaje dhidi ya United? Liverpool watakipiga dhidi ya Manchester United,mchezo huu unaweza kuwa na presha kubwa kwa Jurgen Klopp kutokana na matokeo anayoyapata siku za karibuni huku mshambuliaji muhimu Sadio Mane akiwa majeruhi.
Eneo la ulinzi haliko vizuri na Klopp analijua hilo,tusubiri kuona kama amelifanyia kazi eneo hilo au ataendelea kudoda mbele ya United wanaoonekana kuwa na washambuliaji viwembe.
Romelu Lukaku kuwa mchezaji wa kwanza kuweka rekodi hii? Tayari amefunga katika michezo 7 mfululizo ya Epl na huu ni mchezo wake wa 8 na kama akifunga atakuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika michezo yake 8 ya mwanzo na timu mpya Epl.
United watachezaje bila Pogba na Fellaini? Baada ya Paul Pogba kupata majeraha kocha wa Manchester United alianza kumuamini Marouane Fellaini na sasa Fellaini naye ameumia huku hofu ya majeraha ikianza kuwatesa, Ander Herrera huenda akapewa nafasi na watu wanasubiri kuona nini atafanya.
Tottenham watapata alama 3 kwa mara ya kwanza Wembley? Wembley uwanja wa nyumbani wa Tottenham utawakaribisha Bournemouth, lakini Wembely pamekuwa pagumu mno kwa Tottenham na hawajawahi kupata alama 3 msimu huu na wiki hii wanatari labda wanaweza kuzipata.
Etihad kuendelea kuwa mahala pa kukatili wapinzani? Stoke City anakanyaga Etihad huku wageni wawili waliopita hapa walikula bao tano tano kila mmoja, Stoke wanaenda wakiwa wanayumba yumba nao wanaweza kupata walichopata waliotangulia.
Arsenal wataendeleza vipigo? Michezo minne iliyopita ya Arsenal wanaonekana kuanza kukaa vizuri, Jumamosi hii wataifuata Watford huku Alexis Sanchez akitoka kwenye majonzi ya kulikosa kombe la dunia lakini pia tunasubiri kuona kama Wenger atampa nafasi Wilshaire anayeonekana kutoswa Arsenal.
Brighton watamfukuzisha kazi Ronald Koeman? Ndio/Hapana hili linaweza kutokea, Everton wanaweza kuwa wamechoshwa na matokeo wanayopata ukizingatia kwamba walitumia kiasi kikubwa cha pesa kufanya usajili lakini pia wanaweza kuendelea kumpa muda Koeman aijenge timu.

Raisi wa PSG aingia katika kesi kubwa ya kutoa rushwa


Taifa la Qatar bado linaandamwa na kesi ya rushwa, Qatar wabadaiwa kwamba walitoa rushwa ili wapewe nafasi ya kuandaa michuano ya soka ya kombe la dunia mwaka 2022 suala ambalo liliwaandama sana.
Nasser Al Khelaifi tajiri wa Qatar ambaye ndiye raisi wa klabu ya PSG naye ameingia katika kesi ya rushwa ambapo inadaiwa alitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa moja wa maafisa wa FIFA ili kupewa haki za matangazo.
Al Khelaifi ambaye majuzi tu aliishangaza dunia kwa kufanya usajili uliovunja rekodi ya dunia kumnunua Neymar anadaiwa kwamba alihitaji kumiliki haki za kurusha matangazo ya michezo ya kombe la dunia mwaka 2026 na 2030.
Jerome Vackle aliyekuwa secretary wa zamani wa chama cha soka duniani FIFA anadaiwa alipewa kiasi cha pesa kwa ajili ya kulisaidia shirika la Bein Sports kupata haki za matangazo hayo ya kombe la dunia.
Kuhusishwa kwa Al Khelaifi na kesi hii kunazidi kuiweka Qatar karibu skendo ya rushwa katika fainali za kombe la dunia 2022 ambapo kesi ya Vackle naye ambaye alitimuliwa na FIFA kutokana na kesi za rushwa anazidi kuchafuka.
Maofisa wa masuala ya rushwa kutoka Uswisi wamesema El Khelaifi ambaye ni bosi wa shirika la Bein Sports alilitumia shirika lake kama njia ya kupata tenda hiyo ya matangazo ya kombe la dunia na tayari maofisa hao wameanza uchunguzi dhidi ya Al Khelaifi.
Bado hadi sasa raisi huyo wa PSG hajazungumza lolote juu ya madai dhidi yake japo hii inaweza kuwa kesi kubwa itakayomchafua yeye pamoja na Qatar kuelekea fainali za kombe la dunia mwaka 2022.

Romelu Lukaku ana rekodi mbovu dhidi ya Liverpool na Jose Mourinho ni kibonde wa Klopp, lakini je Liva hii itaweza izuia United ya sasa?


Tangu mwaka 2014 pale Liverpool walipoipiga Manchester United bao 3 kwa 0 klabu hiyo haijawahi kupata ushindi tena dhidi ya Manchester United kwenye mechi zilizofuata za Premier League.
Jumamosi hii wanakutana tena Anfield na safari hii United wanakuja Anfield wakiwa wanajiamini kwanj katika michezo mitano iliyopita waliyocheza hapo United wameshinda mara 3 wakipata suluhu 1 na kupoteza mara 1.
Kama Liverpool wakipoteza mchezo huu itakuwa habari mbaya kwa Klopp kwani 2014 Brenden Rodgers alifukuzwa baada ya kupata alama 12 katika mechi 8 sawa na ambazo Klopp atazipata kama akipoteza mchezo huu.
Lakini Jurgen Klopp anawapa matumaini Liverpool kutokana na rekodi nzuri mbele ya Mourinho kwani katika michezo 7 Mou amemfunga Klopp mara moja tu huku wakisuluhu mara 3 na Klopp akishinda 3.
Manchester United wanaoonekana kutaka kuendeleza wimbi la ushindi wanaweza kuweka rekodi mpya ya kufikisha alama 22 katika michezo 8 ya Epl kama wakiibuka kidedea dhidi ya Liverpool.
United watakuwa na mshambuliaji wao Romelu Lukaku ambaye siku za usoni anaonekana kujenga urafiki na nyavu na kama akifunga atakuwa mchezaji wa kwanza Epl kufunga mfululizo katika mechi 8 za mwanzo.
Lakini pamoja na ukali wake wote wa kufunga Romelu Lukaku huwa anapata wakati mgumu sana mbele ya Liverpool ambapo katika michezo 7 aliyocheza dhidi ya Liverpool amefanikiwa kufunga bao moja tu.
Manchester United watawakosa Paul Pogba na Maroane Fellaini huku ngome yao ya ulinzi ikiwapa jeuri kubwa ambapo kwa mwaka huu tu 2017 wana clean sheets 17 idadi ambayo hakuna klabu waliyoifikia.
Ni mchezo ambao sio mrahisi kwa pande zote kwani Liverpool pamoja na kumkosa Sadio Mane lakini Mo Salah yupo na Coutinho yupo huku United Ander Herrera anaweza kuanza lakini mashaka makubwa yapo katika eneo la ulinzi la Liverpool linaloonekana kupwaya mno, dakika 90 zitaamua.

Kuelekea mpambano wa Liverpool vs Manchester United, Juan Mata afanya jambo kubwa kwa watoto maskini


Manchester United wanakwenda Anfield kuikabili Liverpool Jumamosi hii, mchezo ni mgumu na unataraji kuvuta hisia za watazamaji wengi ulimwenguni kutokana na upinzani na historia baina ya timu hizi mbili.
Wakati wachezaji na mashabiki wakijiandaa na mchezo huu kwa wiki hii, hali ni tofauti kwa kiungo mnyumbulifu wa Manchester United Juan Mata ambaye wiki hii alikuwa na ugeni mkubwa uwanjani Old Traford.
Juan Mata alisafirisha kundi la watoto maskini ambao wanacheza soka kutoka India akawaleta Uingereza ili kuja kuona Old Traford na kupiga picha katika maeneo mbali mbali ya uwanja huo na kujifunza kuhusu soka.
Ziara ya watoto hawa inakuja baada ya miezi michache iliyopita kiungo huyu alipotembelea mji wa Mumbai na kuona mazingira magumu wanayoishi watoto hawa na ndipo aliamua kuwaleta OT kama njia ya kuwahamasisha kufikia malengo yao.
Juan Mata ameamua kuwasaidia watoto hawa kwa kuwahamasisha kuhusu kucheza soka lakini pia kuwapa elimu ya maisha na darasani mpango ambao tayari baadhi ya nyota wakubwa duniani wameanza kumuunga mkono.
Juan Mata aliwaalika Ander Herrera na nyota wa zamani wa United anayekipiga Everton Morgan Schnerdelin kujumuika pamoja na watoto hao pamoja na kupiga nao picha kabla ya kuwapeleka katikati ya uwanja wa Old Traford.
Katika kuendeleza suala hilo Juan Mata amewaomba wacheza soka wenzake kuchangia hata 1% ya kipato chao ili kuwasaidia watoto wasio na uwezo huku akisema anaaamini wachezaji wenzake wa Manchester United watamuunga mkono.
Mlinzi wa Juventus Giorgio Chiellini amemtumia Juan Mata salamu za kumunga mkono kwa kile anachokifanya huku pia Matt Hummels wa Bayern Munich, Serge Gnabry wa Hoffnheim  nao wakiunga mkono kampeni hii ya Juan Matta.

Achana na Liverpool vs United, hii ni michezo 4 ambayo hupaswi kukosa wikiendi hii



Sahau kuhusu Liverpool watakapoikaribisha Manchester United pale Anfield, lakini hii inaweza kuwa wikiendi tamu zaidi katika ligi za barani Ulaya tangu kuanza kwa msimu huu wa 2017/2018.
1.Lyon vs Monaco, wenyeji Lyon wako katika nafasi ya 8 ya ligi na watawakaribisha Monaco walioko nafasi ya 2 katika Serie A, Lyon wamepoteza mchezo mmoja msimu huu sawa na Monaco lakini wamesuluhu mara 3 zaidi ya wapinzani wao.
2.Borussia Dortmund vs Rb Leizp, BvB wamekusanya alama 19 katika michezo 7 ya Bundesliga ikiwa na maana kwamba wameacha alama mbili tu, tangu msimu uanze mwaka huu hawajawahi kudondosha alama 3.
Lakini Rb Leizp wakiongozwa na mshambuliaji anayekuja kwa kasi duniani Timo Werner watajaribu kutafuta ushindi wa 3 mfululizo katika Bundesliga huku wakijiamini kutokana na matokeo mazuri msimu uliopita.
3.Roma vs Napoli, katika michezo 36 waliyocheza klabu ya As Roma wanaonekana wababe wa Napoli ambapo wameshinda michezo 18 kati ya 36 huku Napoli wakishinda michezo 9 na wametoka suluhu mara 9 na wikiendi hii Roma watakuwa Stadio Olimpico kujaribu kuendeleza utemi.
4.Atletico Madrid Vs Barcelona, Diego Simeone ana rekodi mbovu sana dhidi Barcelona ambapo katika michezo 21 amepata ushindi mara mbili tu na safari hii anawakaribisha Barcelona ambao msimu huu wanaonekana hawashikiki.
Barcelona wamekusanya alama zote 21 katika michezo yao 7 katika La Liga huku Atletico walioko nafasi ya 4 nao hawajapoteza mchezo hata mmoja lakini wamesuluhu mara 3 na kupata jumla ya alama 14.

Msiompenda Cr7, rekodi zinaonesha huu ni mwezi mbaya kwenu


Msimu wa La Liga umeanza vyema kwa Lioneil Messi na Barcelona huku upande wa pili Cristiano Ronaldo akianza kwa kusua sua katika michuano hii ya La Liga jambo linalowaumiza mashabiki wake.
Lakini rekodi hazidanganyi na rekodi zinaonesha kwamba mwezi huu wa 10 huwa ndio mwezi ambao Mreno huyu huutumia kufanya makubwa na ndio mwezi ambao wapinzani wa Ronaldo huteseka.
Mwaka 2010 mwezi kama huu Cr7 alifunga hatrick nne na 2011 mwezi wa 10 Cristiano Ronaldo aliweka rekodi baada ya kufunga mabao 10 katika michezo 4 ya ligi kuu nchini Hispania La Liga.
Msimu wa mwaka 2014/2015 katika mechi mbili za La Liga Cr7 aliweka kambani bao 6 na kudhihirisha kwamba yeye ndio mfalme wa mwezi October.
Malaga wamekuwa wahanga wakubwa wa Cristiano Ronaldo katika mwezi wa 10 ambapo amewafunga mara 6, wakifuatiwa na Levante aliowaua mara 4 huku Barcelona,Sevilla, Alaves akiwafunga mara tatu tatu.
Mwezi huu Eibar, Girona na Getafe watakutana na Cr7 huku Tottenham Hotspur nao watakutana na Cristiano Ronaldo katika mwezi ambao anaogopesha na kwa kuanzia wataanza Gdtafe siku ya Jumamosi.

Hiki ndicho kilichopelekea Pochettino kusema “Gurdiola hana nidhamu na anapenda kuwadharau wenzake” 



Kocha wa klabu ya Tottenham Hotspur Maurcio Pochettino ameonekana kuchukizwa na maneno yaliyotolewa na Pep Gurdiola na kusema hadharani kwamba anahisi kukosewa heshima na kocha huyo.
Haya yamekuja baada ya Pe Gurdiola kuipa Tottenham Hotspur jina jipya la “Timu ya Harry Kane” kitendo ambacho Pochettino amekitafsiri kama muendelezo wa Pep Gurdiola kudharau watu wengine.
Pochettino amesema anamjua vyema Pep Gurdiola tangu kabla hajajiunga na Barcelona na anaamini katika uwezo wa kocha huyo lakini anafahama Pep hana nidhamu na amekuwa hivyo kwa watu wengi.
Pochettino amesema anashangazwa sana na kitendo cha kocha huyo kuwaita “Timu ya Kane” wakati yeye mafanikio yake makubwa alipokuwa Barcelona yaliletwa na Lioneil Messi lakini hakuna aliyewaita “Timu ya Lioneil”
Pochettino amesema mafanikio ya timu sio mtu mmoja na maneno kama aliyosema Gurdiola yanawakera watu wengi na wengi wanajisikia vibaya na kuchukulia maneno hayo kama ukosefu wa nidhamu.
Kocha huyo wa Tottenham amesema wakati wa mapumziko katikati ya wiki alikuwa kimya akiamini Pep atampigia simu kuomba msamaha lakini kocha huyo hakufanya hivyo lakini akisema hilo halijawaathiri wachezaji wameishia kucheka.
Harry Kane amekuwa na misimu mizuri sana siku za usoni huku msimu huu akiwa ameweka kambani magoli 15 katika michezo 10 na pia akifunga mabao 11 kati ya 16 ya Tottenham msimu huu hali inayowafanya wengi kuamini anaibeba Tottenham.

Hakuna maoni: