Mambo matano niliyoyaona EPL Jumamosi hii
1.United wanazuilika kabisa, ilikuwa suluhu 3 ambayo haikuwa na mabao kati ya Liverpool na Manchester United, lakini mchezo wa leo Anfield umeonesha United wanaweza kuzuilika kabisa huku walinzi wa Liverpool wakimpoteza nyota wao Romelu Lukaku,ni wazi United kama sio De Gea wangekufa.
Katika suluhu hiyo mlinzi wa kulia wa Manchester United Antonio Valencia aliweka rekodi kuwa mchezaji wa kwanza ambaye sio mzaliwa wa bara la Ulaya kuichezea United michezo 300.
2.Chelsea kama popo, Goli la kuongoza la Crystal Palace liliwafanya Palace kukomesha njaa yao ya ufungaji ambayo imedumu kwa muda wa masaa 12 na hilo lilikuwa bao lao la kwanza kupata katika mashuti 86 waliyopiga msimu huu.
Chelsea msimu huu imekuwa haieleweki kwani kuna wakati wanaonekana wamechoka sana lakini kuna wakati wanaonekana kujaribu kurudi, kipigo cha leo kimewarudisha nyuma kwani wangeshinda wangepunguza pengo la alama na timu zilizoko juu yao.
3.Pep anataka kombe tu sio hadithi, Etihad panaonekana sasa sio mahalinpakwenda kabisa, wapinzani, timu mbili kabla ya Stoke zilizofika Etihad zilikufa bao 5 huku leo Stoke City akila 7 kwa 2 ambazo kwa mahesabu mengine ni sawa na 5 bila, usajili aliofanya na matokeo anayopata vinaonesha wazi anataka ndoo.
4.Wenger arudi kwenye sack race, Arsenal Wenger ameanzishiwa tena mabango ya Wenger Out ambayo yalishaanza kupotea, kipigo cha bao 2 kutoka kwa Watford kimeamsha hisia kali kwa mashabiki wa klabu hiyo na wameshaanza kutuma ujumbe wa Wenger out mitandaoni na sasa anarejea katika mbio za kufukuzwa.



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni