tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

11 Oktoba 2017

Netflix waingia mkataba na Juventus utakaowaumiza Manchester United na Barcelona


Kampuni inayohusu masuala ya kustream movie online ya Netflix imeingia ubia na klabu bingwa ya nchini Italia klabu ya Juventus na sasa wanakuja na jambo bora kwa ajili ya mashabiki wa soka watumiaji wa mtandao huo.
Netflix wameamua kutengeneza video ihusuyo maisha ndani ya wababe hao wa Italia (Documentary) ambapo ndani ya Documentary hiyo watazamaji watapata kuona karibia kila kitu ndani ya klabu hiyo.
Documentary hiyo itaonesha mechi za Juventus lakini pia itakuwa inaonesha matukio mbali mbali yanayotokea wakati Juventus wakiwa mazoezini, wakiwa vyumba vya kubadilishia nguo na wakiwa safarini.
Makamu mwenyekiti wa Juventus Federico Palomba amejinadi kwamba kwao hayo ni mafanikio makubwa sana na wao kama Juventus wanajisikia faraja kubwa kuwa klabu kubwa ya kwanza duniani kufanya hivyo.
Naye makamu wa raisi wa Juventus Erick Barmack anaamini klabu kama Juventus ina historia kubwa ambayo dunia inapaswa kuifahamu na kupitia Netflix itakuwa rahisi kwa ulimwengu kuijua Juventus.
Wakati Juventus wakiingia mkataba na Netflix inaonekana wazi itakuwa ngumu sana kwa sasa kumruhusu Paulo Dyabala kuondoka, hii inatokana na sababu kwamba ili documentary iangaliwe zaidi ni lazima kuwepo kwa wachezaji wakubwa.
Kulikuwa na tetesi kwa Paulo Dyabala kuihama klabu hiyo na kutimkia Barcelona au Manchester United lakini sasa ni inaonekana itakuwa ni ngumu zaidi kwa Juventus kumuacha aondoke kwani wanamuhutaji sio tu uwanjani bali na kuitangaza klabu.

Hiki ndicho kikosi bora kitakachoangalia kombe la dunia videoni


Lioneil Messi alfajiri ya leo ameipeleka Argetina katika michuano ya kombe la dunia mwakani, hii inaifanya michuano hii kuwa na Cristiano Ronaldo na Lioneil Messi lakini kuna wachezaji 11 wakubwa ambao wanakosa michuano hii.
Jan Oblak. Akiwa na miaka 24 tu tayari mlinda lango huyu anatajwa kama kati ya makipa bora kuwahi kutokea La Liga, pamoja na ubora wake lakini ameshuhudia Slovenia ikikosa michuano ya kombe la dunia.
Antonio Valencia. Mlinzi wa kulia wa Manchester United ambaye ni kati ya wachezaji tegemezi Ecuador, alfajiri ya leo wamekula bao 3 lakini hata kabla walikuwa tayari wameshakosa tiketi.
David Alaba. Upande wa kulia yupo Alaba ambaye anacheza katika kiwango cha juu sana akiwa na Bayern Munich lakini pamoja na uwezo wake ameshindwa kuisaidia Austria kwenda Urusi mwakani.
Virgil Van Dijk. Katika dirisha hili la mwisho la usajili jina lake limekuwa likitajwa sana kutokana na uwezo wake lakini yeye na Uholanzi hawajafanya jambo kubwa la kuwapa tiketi kwenda kombe la dunia.
Gary Medel. Hili linaweza kuwa jina kubwa kwa wengine lakini Medel anayeichezea Bestikas kwa sasa ni kati ya walinzi hodari sana katika bara la Ulaya hivi sasa,  lakini ameshindwa kuizuia Chile isitolewe.
Naby Keita. Mashabiki wa Liverpool wanamjua vyema huyu kiungo kutokana na walivyohangaika kumpata, lakini baada ya Guinea kukosa tiketi ya kombe la dunia ina maana Keita ataangalia michuano hiyo kideoni.
Artulo Vidal. Kiungo mwingine wa kati kutokea Bayern Munich, Vidal ana uwezo mkubwa sana uwanjani lakini ameiangusha Chile katika kufuzu kwenda kombe la dunia.
Gareth Bale. Nyota wa kiwango cha dunia anayekipiga Real Madrid, wakati CR7 anakwenda kombe la dunia itabidi Bale aangalie tu baada ya Wales kushindwa kufuzu.
Christia Pulisic. Huyu anaitwa Lioneil Messi wa Marekani, yupo katika kiwango kikubwa sana lakini pamoja na kufunga bao moja alfajiri lya leo alishuhudia Panama wakikata tiketi kwenda Urusi.
Alexis Sanchez. Mwanazoni alikuwa na matumaini kwenda kombe la dunia lakini kipigo cha bao 3 toka kwa Brazil kilikata ndoto na matumaini ya mshambuliaji huyu wa Brazil.
Pierre Aubemayang. Anaongoza katika ufungaji Bundesliga lakini ameshindwa kuiongoza Gabon kwenda kushiriki kombe la dunia, hadi sasa iko wazi kwamba Aubemayang hatakwenda Urusi kushiriki kombe la dunia.

Ureno na Ufaransa  wakata tiketi ya Urusi 2018

Andre Silva alifunga moja kati ya mabao mawili wakati Ureno wakiipiga Switzland bao 2 na hii inamfanya mshambuliaji huyu kuhusika katika mabao 10 kwenye michezo 10 ya timu ya taifa ya Ureno.
Na ushindi wao wa leo ni mafanikio mengine kwao na kwa mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo kwani Wareno wanakuwa wamekata rasmi tiketi ya kushiriki kombe la dunia.
Hii ni mara ya 9 mfululizo kwa Ureno kushiriki kombe la dunia huku safari hii wakiwa wamefunga jumla ya mabao 32 na wakiwa na clean sheets katika michezo 7.
Timu ya taifa ya Ufaransa nayo imewapiga Belarus bao 2 kwa 1 na kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia huku wakiweka rekodi ya kutopteza mchezo hata mmoja katika uwanja wao wa nyumbani wakati wa mechi za kufudhu.
Kule Ubelgiji nako watoto wawili kutoka familia moja ya mzee Hazard walishirikiana kuendeleza utemi wa Ubelgji, huyu ni Eden Hazard alyefunga mara mbili huku Thorgan akifunga moja na Lukaku akimalizia la nne dhidi ya Cyprus.
Kwa ushindi huu wa mabao manne huku magoli mawili kutoka kwa Eden Hazard yanmfanya hadi sasa kuhusika katika mabao 9 ya Ubelgiji katika michezo 10 akigunga manne na kuassist 5.
Michezo mingine ya Group H timu ya taifa ya Ugiriki ilishinda mabao 3 kwa 0 dhidi ya Gibrtar huku mabao ya Ugiriki yakiwekwa kimiani na K Mitroglou (2) na Torosidis.
Timu ya taifa ya Uholanzi imekwama kufuzu kwa michuano ijayo ya kombe la dunia licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Sweden lakini haikutosha kuwapeleka kombe la dunia.


 

Hakuna maoni: