tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

6 Oktoba 2017

Wakati wakijiandaa dhidi ya N Ireland, mchezaji wa Ujerumani aweka rekodi Epl



Hii leo michezo ya kufudhu kwa fainali za kombe la dunia zitakazopigwa nchini Urusi mwakani inaendelea, Ujerumani vinara wa Group C watakuwa ugenini kuwakabili Northern Ireland 
Wakati Wajerumani wakijiandaa na mchezo huo, mchezaji wao kinda anayekipiga Manchester City ameweka rekodi Epl, Leroy Sane ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye kasi zaidi rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Jamie Vardy.
Katika mchezo dhidi ya Chelsea ambapo Man City waliibuka kidedea, winga huyo alikimbia kilomita 35.48 kwa lisaa akimzidi Jamie Vardy ambaye alikimbia kwa kilomita 35.44 kwa saa zima.
Kwa msimu huu anayemfuatia Leroy Sane ni mchezaji wa klabu ya Crystal Palace Patrick Van Anholt ambaye amekimbia kilomita 35.42 kwa lisaa na baada ya Anholt anayefuatia ni beki wa Chelsea Antonio Rudiger ambaye pia ni Mjerumani akikimbia kilomita 35.19.
Kyle Walker ambaye timu yake ya taifa ya Uingereza inashuka dimbani usiku huu dhidi ya Slovenia yuko nafasi ya nne akikimbia kilomita 35.16 kwa saa huku Oliver Burke akishika nafasi ya 5 akikimbia kilomita 35.13 kwa saa.

Harry Kane aipeleka Uingereza nchini Urusi, Lewandoski naye aweka rekodi ya mabao


Michezo 90 aliyoichezea Poland Roberto Lewandoski amefunga mabao 50 ikiwemo matatu ya usiku wa leo wakati wakiiua Armebia waliokuwa nyumbani kwa jumla ya mabao 6 kwa goli moja.
Roberto Lewandoski huyo huyo ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 15 katika michezo ya kufudhu fainali za kombe la dunia, mabao mengine ya Poland yalifungwa na Grosicki, Rafal Wolski na Jakub.
Ujerumani wakaendelea kutembeza kichapo cha mabao 3 kwa 1 dhidi ya Northen Ireland matokeo ambayo yanawafanya kutopoteza mchezo wowote katika michezo 18 iliyopita tangu walipofungwa na Ufaransa Euro 2016.
Ujerumani wanakuwa wamecheza michezo 10 bila kuruhusu bao wakiruhusu katika michezo 9 huku wakifunga jumla ya mabao 54, katika mchezo wa leo mabao ya Ujerumani yaliwekwa kimiani na Sabastian Rudy, Sandro Wagner na Joshua Kimmich.
Bao la Harry Kane dakika ya 90 lilipeleka shangwe kwa malkia Elizabeth na kuwafanya Waingereza kufudhu kucheza fainali za kombe la Dunia mara 6 mfululizo huku uwanja wa Wembley ukiwabeba katika michezo 14 yote iliyopita wakiibuka kidedea.
Norway waliipiga San Marino mabao 8 yaliyofungwa na Joshua King(2), Mohamed Elyounoussi(3),Marcus Herricksen,Martin Linnes na Kristina Selnaes, hii ni mara ya kwanza kwa Norway kufunga idadi hiyo ya mabao katika karne ya 21.
Christian Erriksen aliisaidia Dernamark kuichapa Montenegro bao 1 kwa nunge huku Malta na Liuthania wakiondoka na sare ya moja kwa moja, Czech nao wakiwa ugenini waliipiga Azerbaijan bao 2 kwa 1 huku mabao ya Czech yakifungwa na  Jan Kopic na Athony Barak.

Nani kuiwakilisha Afrika kombe la dunia 2018?


Kuna nafasi 5 za Afrika kwenda katika michuano ya kombe la dunia itakayopigwa nchini Urusi mwakani. Lakini hadi hivi sasa upatikanaji wa nafasi hizo umekuwa mgumu sana na hakuna mwenye uhakika kwenda Urusi.
Group A kuna timu za Guinea, Libya, Tunisia na Dr Congo huku tayari Guinea na Libya hawana nafasi. Tunisia na Dr Congo wanapigania kupata nafasi moja tu huku Tunisia wakihitaji alama 4 tu kuipata nafasi hiyo,michezo ya Group hii itapigwa siku ya Jumamosi ambapo Guinea atakipiga dhidi ya Tunisia huku Libya wataikaribisha Dr Congo.
Group B nako Zambia na Nigeria ndio waliobaki kupambania nafasi ya kwenda kombe la dunia huku wakikutana Jumamosi mchezo ambao unaweza kuamua anayekwenda Urusi, lakini Algeria na Cameroon wenyewe hawana nafasi tena na watakutana Jumamosi.
Group C. Mali, Ivory Coast, Gabon na Morocco wapo katika kundi hili, kati ya makundi yote hili lina mvuto mkubwa kwani timu zote nne zina matumaini kwenda Urusi mwaka 2018, Ivory Coast na Morocco wote wanahitaji alama 6 kwenda Urusi na Jumamosi wanakutana katika mchezo mgumu zaidi kufudhu kombe la dunia ukanda wa Afrika.
Group D, kama ilivyo kwa Group C hili nalo ni group ambalo wote wana nafasi. Burkina Fasso wako kileleni mwa kundi kwa tofauti ya mabao lakini Cape Verde nao hawako mbali na kileleni huku timu mbili za mwisho Senegal na Bafanabafana wote wakishinda michezo iliyobaki wana nafasi. 
Group E, group pekee lenye timu kutoka Afrika Mashariki, Egypt wanaongoza kundi hili na alama 9 huku Uganda wakiwa na 7, Ghana wako na tano na Wacongo tayari hawana nafasi, Jumamosi hii Uganda wataikaribisha Ghana na huku Egypt wakikipiga na vibonde Congo.

Lioneil Messi watatu ni Cr7 mmoja sokoni


Pesa ndio kila kitu, hakuna kinachoshindikana unapokuwa na pesa. Kwani ni nani aliyewaza kwamba siku moja kuna timu kutoka Ligue 1 ambayo itatoa kiasi cha €220m kwa ajili ya kumnunua Neymar.
Vilabu vya soka nchini Hispania vinaelewa fika kwamba wachezaji wao wanatamaniwa na vilabu vingi duniani, walichoamua kufanya Wahispania ni kuweka kiasi cha pesa katika mikataba ambapo kama unamtaka mchezaji inabidi ukitoe.
Cristiano Ronaldo yuko kieleleni katika wachezaji ambao ukiwataka itakubidi utoe kiasi kikubwa, Real Madrid wameweka kiasi cha £886m kwenye mkataba wa Ronaldo pesa ambayo ni karibia mara nne ya kiasi alichonunuliwa Neymar.
Baada ya Cr7 chini yake yupo mchezaji mwingine wa Real Madrid Karim Benzema ambapo Benzema ukimtaka unatakiwa kutoa kiasi sawa na kiasi cha kumnunua Cristiano Ronaldo cha £886m.
Marco Asensio. Kati ya makinda ambao wanazungumzwa sana duniani ni Marco Asensio na Real Madrid wanalijua hilo na ndio maana haikuwa tabu kwao kuweka kiasi cha £620m kama unamtaka kiasi ambacho ni sawa na kiasi cha kumpata Isco.
Gareth Bale na Toni Kroos ambao wote ni moja kati ya wachezaji wanaotafutwa na Manchester United lakini inahitajika kiasi cha £443m kuwang’oa Real Madrid pesa ambayo ni sawa na Luca Modric.
Katika hali ambayo si ya kawaida mpinzani mkubwa wa Cr7 ambaye ni Lioneil Messi anauzwa bei ndogo sana tofauti na Cr7 ambapo Barca wanahitaji £266m tu kiasi ambacho ni karibia mara 4 ya kiasi cha kumnunua Cr7.
Antoine Griezman ambaye naye pia anahitajika Old Traford na kama kweli United wanamtaka baaai inatakiwa watoe kiasi cha £177m, kiasi hicho cha pesa ni sawa pia na pesa ya kumng’oa Andres Iniesta na Luis Suarez.
Ada za uhamisho kuwanunua wachezaji zimekuwa zikikua siku hadi siku na rekodi za uhamisho zikivunjwa kila msimu ambapo kwa sasa striker wa PSG Neymar ndio anashikilia rekodi ya uhamisho wa dunia baada ya Barca kumuuza kwa £220m.

Wakiwa kwenye vita ya miaka 6 – Syria kujifuta machozi na kufuzu kombe la Dunia?


Wakati miji mbalimbali ya nchi hiyo ikiwa katika hali mbaya na mamilioni ya wananchi wake wakiwa wanapigika kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe, Syria wanapigana kufanikisha ndoto ya kushiriki katika michuano ya kombe la dunia 2018.
Wakiwa hawapewi nafasi kabisa, kikosi cha timu ya taifa ya Syria kinachoshika nafasi ya 75 ya ubora duniani, kimeushangaza ulimwengu wa soka duniani kwa kuwavimbia na kutoka sare na timu kama Korea ya Kusini na Iran, wamewafunga China, Qatar na Uzbekistan – matokeo ambayo yaliwapa nafasi ya pili katika kundi lao na nafasi ya kucheza play-off.
Wasyria wanaojulikana kwa jina la “Qasioun Eagles” walipata taabu kukabiliana na michezo ya kundi lao – wakicheza mechi zao za nyumbani katika ardhi ya Oman na Malaysia.
Leo jioni wamepata sare dhidi ya Australia, wametoka sare ya 1-1 katika mchezo uliopigwa nchini Malaysia. Sasa mchezo huo utarudiwa nchini Australia na mshindi atacheza dhidi ya mshindi wa 4 wa kundi la CONCACAF qualifiers, ambaye huenda akawa Panama, Honduras au hata Marekani.
Mpaka kufikia hapa Syria wamepambana kuvuka vikwazo vyote, nchi yao ikiwa imegubikwa na vita ambayo imeshachukua uhai wa watu 470,000 na wengine mamilioni wakiwa hawana makazi ya kuishi – kwa mujibubwa shirika la haki za binaadamu la Uingereza ambalo limesema mwezi September umekuwa mwezi ambao damu imemwagika zaidi katika vita hiyo iliyodumu kwa miaka 6 sasa.
Vikosi vya kijeshi vya Syria – vinavyomsapoti Rais Bashar al-Assad, sasa vinashikilia maeneo mengi ya mjini kufuatia mapigano ya miaka 4 katika eneo la Aleppo, mji wa pili kwa ukubwa wa nchi hiyo – na sasa vikosi vya jeshi vinajiandaa kwa pambano la mwisho dhidi ya kikundi cha Islamic State (ISIS) kwa ajili ya kuchukua eneo la Deir Ezzor.
Rais Assad, ambaye amekuwa akituhuhumiwa kuhusika makosa ya jinai ya kivita – anaripotiwa kuwa shabiki mkubwa wa Qasioun Eagles, jambo limepelekea watu kadhaa kuhisi kama huenda mafanikio ya timu ya taifa yakatumika kisiasa.
Lakini wachezaji wa Syria wanasema hakuna anayejihusisha na masuala ya siasa.
“Hatujihusishi kabisa na masuala ya siasa,” anasema mshambuliaji Firas Khatib alipokuwa akiongea na gazeti la Times. “Tunajituma kuhakikisha tunamwakilisha kila raia wa Syria.”
Nafasi ya kuweza kufuzu kucheza kombe la dunia imekuwa jambo lenye hisia kubwa kwa Wasyria ambao wengi wao wanaugulia maumivu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.
Tarehe 10, mwezi huu – mamilioni ya wananchi wa Syria watasimama kwa dakika 90 kuiombea kheri timu yao katika mchezo wa marudiano dhidi ya Australia ili kuamua timu itakayopata nafasi ya kwenda kucheza na mshindi kutoka CONCACAF.

Brazil walazimika kutumia mashine maalum za kupumulia baada ya kubanwa na Bolivia


Jana michuano ya kufudhu kwa faiinali za kombe la dunia zitakazopigwa nchini Urusi ziliendelea, katika bara la America Kusini michezo mbali mbali ilipigwa lakini vinara wa bara hilo Brazil walikutwa na makubwa baada ya mechi yao.
Brazil waliokuwa wakicheza dhidi ya Bolivia walitoka suluhu ya bila kufungana lakini hiyo haikuwa habari kubwa kama habari ya wachezaji wa Brazil kutumia mask za Oxygen ili kuweza kupumua.
Uwanja wa Estadio Hernando upo 4000m kutoka usawa wa bahari hali inayoifanya eneo hili kuwa na kiwango cha juu sana cha joto tofauti na mji mkuu wa Brazil wa Rio Di Jeneiro.
Dani Alves, Neymar, Gabriel Jesus na Paulinho ni moja kati ya nyota ambao walipata wakati mgumu kupumua na kuonekana wakiwa wamevaa mask hizo ili kuwasaidia kupata hewa.
Mchezaji ghali duniani Neymar Dos Santos ameitaja hali ya hewa ya Bolivia kama hali mbaya sana kuwahi kucheza soka siku za karibuni na kusema hawakufurahia kabisa mazingira ya mchezo huo.
Hali hii imekuja siku moja baada ya mchezaji wa Ecuador Antonio Valencia kuonya kwamba kati ya vitu vinaifanya michuano ya bara hilo kuwa migumu ni kutokana na hali tofauti ya hewa ambayo inaweza kusumbua wachezaji.
Lakini pamoja na hali hiyo mbaya lakini haikuwazuia Brazil kupata alama moja iliyofanya kufikisha idadi ya michezo 11 bila kupoteza huku ikiwa timu pekee kushiriki fainali zote za kombe la dunia tangu mwaka 1930.

Andres Iniesta awa mchezaji wa kwanza kusaini mkataba wa milele


Tarehe 6 mwezi October mwaka 1996 ndio kwa mara ya kwanza Andres Iniesta alianza kuitumikia Barcelona, kuanzia hapo kilichoendelea ni historia akibeba makombe 30 katika michezo 639.
Kumekuwa na habari nyingi za hivi karibuni zikimuhusisha Iniesta ambapo ilisemekana kwamba kiungo huyo anaweza asimwage wino katika klabu hiyo kutokana na mazungumzo ya mkataba kuchukua mda mrefu huku mkataba alionao kuisha mapema mwakani.
Baada ya habari hizo hii leo Andres Iniesta amewaziba watu midomo kabisa baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kusaini mkataba wa maisha, inamaanisha Iniesta amesaini mkataba utakaomuweka Barca hadi anastaafu soka.
Iniesta mwenye miaka 33 kwa sasa, alikuwepo Barcelona tangu akiwa na miaka 12 lakini alikuwa akiichezea timu ya vijana na ilipofika mwaka 2002 Mhispania huyo kwa mara ya kwanza alichezea timu ya wakubwa.
Klabu ya Barcelona imesema kwa miaka 118 ya Historia ya klabu hiyo wasingependa kuona kizazi cha dhahabu kama cha wakiana Iniesta kupotea kirahisi na ndio maana haikuwa ngumu kumpa mkataba wa milele na usiokuwa na mwisho.
Andres Iniesta baada ya kusaini mkataba huo amesema kwamba kubaki hapo ndio ilikuwa ndoto yake na pamoja na miaka 33 aliyonayo lakini hajawahi kuwaza kufanya kitu kingine zaidi ya kubaki Nou Camp.

Hakuna maoni: