tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

27 Januari 2015

AFCON 2015: TUNISIA, CONGO DR ZASONGA, CAPE VERDE, ZAMBIA NJE!!

AFCON2015-SSKUNDI B la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, limecheza Mechi zao za mwisho ambazo zote mbili ziliisha kwa Sare ambazo zimewanufaisha Tunisia na Congo DR kutinga Robo Fainali huku Cape Verde na Zambia wakitupwa nje.
Kwenye Robo Fainali, Tunisia watawavaa Wenyeji Equatorial Guinea na Congo DR kucheza na Jirani zao Congo.
CONGO DR 1 TUNISIA 1
>>Estadio de Bata, Mjini Bata
Tunisia na Congo DR zimefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, baada ya kutoka 1-1 katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi A iliyochezwa huko Estadio de Bata, Mjini Bata.
Ahmed Akaichi aliwapa Bao Tunisia kwa Kichwa katika Dakika ya 31 baada kuunganisha Mpira uliopigwa na Chikhaoui.
Congo DR walisawazisha Dakika ya 66 baaada ya Mpira mrefu kunaswa na Mbokila aliemshushia Loteteka Bokila aliefunga.
VIKOSI:
Congo DR: Kidiaba, Mbemba, Kimwaki, Issama, Kasusula, Mongongu, Makiadi, Bolasie, Cedrick, Mubele, Mbokani.
Akiba: Kudimbana, Oualembo, Munganga, Kage, Kebano, Mabele, Kabananga, Zakuani, Bokila, Mabidi, Mandanda.

Tunisia: Aymen Mathlouthi, Yacoubi, Syam Ben Youssef, Maaloul, Hamza Mathlouthi, Abdennour, Khazri, Sassi, Ragued, Akaichi, Chikhaoui.
Akiba: Ben Mustapha, Mohsni, Bedoui, M’Sakni, Fakhreddine Ben Youssef, Younes, Chermiti, Nater, Moncer, Saihi, Ben Djemia, Ben Cherifia. 
Refa: Bakary Gassama (Gambia) 
CAPE VERDE ISLANDS 0 ZAMBIA 0
>>Nuevo Estadio de EbebiyĆ­n, Mjini Ebebiyin
Cape Verde na Zambia wametoka 0-0 katika Mechi yao ya mwisho ya Kundi B la AFCON 2015 huko Mjini Ebebiyin Nchini Equatorial Guinea na wote kutupwa nje kufuatia Sare ya 1-1 ya Mechi nyingine ya Kundi A ambayo iliwapitisha Tunisia na Congo DR.
VIKOSI:
Cape Verde: Vozinha, Fernando Varela, Carlitos, Stopira, Gege, Toni Varela, Rocha, Lima, Heldon, Rodrgues, Ryan Mendes.
Akiba: Sousa, Kay, Babanco, Semedo, Odair Fortes, Kuca, Platini, Tavares, Nivaldo, Djaniny, Jeffrey Fortes, Somada.

Zambia: Mweene, Sunzu, Nkausa, Munthali, Mbola, Mtonga, Kalaba, Lungu, Musonda, Singuluma, Kangwa.
Akiba: Munyao, Malama, Kabwe, Sautu, Musakanya, Kampamba, Mulenga, Mwanza, Ngoma, Titima.
Refa: Neant Alioum (Cameroon)


Hakuna maoni: