tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

27 Januari 2015

CAPITAL ONE CUP-NUSU FAINALI: JUMANNE USIKU NI MARUDIANO STAMFORD BRIDGE CHELSEA v LIVERPOOL!

CAPITAL-ONE-CUPBAADA ya kutoka Sare 1-1 huko Anfield katika Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe la Ligi, sasa maarufu kama Capital One Cup, Chelsea na Liverpool zitarudiana Uwanjani Stamford Bridge Jumanne Usiku Januari 27.
Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Wiki iliyopita, Chelsea walitangulia kufunga kwa Penati ya Eden Hazard katika Dakika ya 18 na Raheem Sterling kuisawazishia Liverpool kwenye Dakika ya 59.
Kwenye Nusu Fainali, Kanuni muhimu inayotumika ni ile ya kupata Mshindi ikiwa Timu zìtakuwa Sare na pia kufungana kwa Magoli sawa katika Mechi zao 2 baada ya Dakika 90.
Hali ikiwa hivyo, bila ya kuhesabu Magoli ya Ugenini, utachezwa Muda wa Nyongeza wa Dakika 30 na baada ya muda huo, ikiwa Mechi bado ni Sare, basi ile Sheria ya Bao la Ugenini kuhesabika Mawili ndiyo itatumika.
Na endapo, wakati huo, hata ikitumika Sheria ya Bao la Ugenini kuwa Mawili bado Timu zinabaki Sare, Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati 5.
Katika Nusu Fainali nyingine ambayo Mechi ya kwanza ilichezwa pia Wiki iliyopita huko White Hart Lane, Tottenham iliifunga Sheffield United Bao 1-0 kwa Bao la Penati iliyotolewa Dakka ya 75 baada ya Jay McEveley kuushika Mpira na Andros Townsend kupiga Penati hiyo na kufunga.
Marudiano ya Sheffield United na Tottenham ni hapo Jumatano Januari 28 Nyumbani kwa Sheffield.
CAPITAL ONE CUP
RATIBA
++Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku, Bongo Taimu
Marudiano
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Jumanne Januari 27
Chelsea v Liverpool [1-1]
Jumatano Januari 28
Sheffield United v Tottenham [0-1]      
++++++++++++++++++++++++++++++
FAINALI
Jumapili 1 Machi 2015
Liverpool au Chelsea v Tottenham au Sheffield United
++++++++++++++++++++++++++++++
****FAHAMU:
-Kwenye Nusu Fainali, ikiwa Timu zìtakuwa Sare na pia kufungana kwa Magoli katika Mechi zao 2, utachezwa Muda wa Nyongeza wa Dakika 30.
-Baada ya muda huo, ikiwa Mechi bado ni Sare basi ile Sheria ya Bao la Ugenini kuhesabika Mawili itatumika.
-Endapo hata ikitumika Sheria ya Bao la Ugenini kuwa Mawili bado Timu zinabaki Sare, Mshindi atapatikana kwa Mikwaju ya Penati 5.

Hakuna maoni: