AARIFA TAMU KWA MASHABIKI WA ARSENAL KUHUSU ARTURO VIDAL
Wakati huu mashabiki wa Arsenal
wakisubiri golikipa wa Chelsea, Petr Cech kujiunga Emirates, kuna
taarifa mpya kwamba kiungo wa Chile na Juventus, Arturo Vidal naye yuko
mbioni kutua Kaskazini mwa London.
Vidal ambaye anaitumikia Chile
katika michuano ya Copa America inayoendelea katika ardhi yao, kwa muda
mrefu amekuwa akihusishwa kutua England hususani katika klabu ya
Manchester United.
Leo tetesi zimeibuka kwamba
Vidal ataondoka Juventus majira haya ya kiangazi na tayari amekubali
dili la kujiunga na Arsenal ambalo litatangazwa baada ya Copa America
kufikia tamati.
Tetesi hizo zimeibuka saa
chache zilizopita kutoka kwa Mwandishi wa habari wa Chile, Hernan Feler
ambayo amethibitisha kwenye radio kwamba Arsenal wamemsajili Vidal.
Feler ni chanzo makini cha
habari? bado haijulikani, lakini idadi kubwa ya mashabiki wa Arsenal
wanadai ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza taarifa za Alexis Sanchez
kutua Arsenal kutokea Barcelona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni