ARTURO VIDAL ASHAUZWA!
Hivi sasa Vidal, ambae Wiki iliyopita huko kwao Chile alifunguliwa
mashitaka ya kuendesha Gari huku akiwa amelewa na kusababisha ajali,
yuko huko huko Chile akiichezea Nchi yake inayoshiriki Copa America
ambapo Jumanne Usiku itacheza Nusu Fainali na Peru.
Licha ya Marca kudai Klabu ambayo Juve imemuuza Vidal ni siri,
habari zilizozagaa zinadai Mchezaji mwingine wa Chile anaechezea
Arsenal, Alexis Sanchez, ndie aliemfanya Vidal aamue kwenda Arsenal.
Vidal ni mmoja wa Wafungaji Bora wa Copa America akiwa na Bao 3 na
alianzia Soka lake la Kulipwa akiwa na Klabu ya Colo-Colo ya Chile Mwaka
2005 hadi 2007 alipohamia Bayer Leverkusen ambako alicheza Mechi 117 na
kufunga Bao 15 kisha Mwaka 2011 kwenda Juventus alikocheza Mechi 124 na
kufunga Bao 35.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni