BAADA KUTUPWA NJE, DUNGA ADAI COPA AMERICA HAINA 'MAANA YEYOTE!'
Brazil ilitupwa nje kwenye Robo Fainali ya Copa America na Paraguay
baada kutoka Sare 1-1katika Dakika 90 na kushindwa kwa Mikwaju ya
Penati 4-3 huku wakicheza bila ya Kepteni wao Neymar aliefungiwa baada
ya Mechi ya PIli ya Kundi lao la Mashindano hayo baada ya kupewa Kadi
Nyekundu kwenye Mechi na Colombia.
Dunga ameeleza: "Brazil ilikwenda Miaka 40 bila Copa America [1949
hadi 1989] na tulikuwa tukishinda kwingineko. Halafu tukaanza kushinda
Copa America [Mataji 5 tangu 1989] na tukaambiwa Kombe hilo halina
maana, muhimu ni Kombe la Dunia."
Aliongeza: "Tulipocheza Kombe la Mabara na kushinda, tukaambiwa
halina maana. Sasa Vyombo vya Habari vimeamua Copa America ni muhimu.
Soka ndio ilivyo!"
Akiwa kama Mchezaji, Dunga alitwaa Copa America mara 2 [1989 na
1997] na kisha kulibeba akiwa Kocha wa Brazil Miaka 8 iliyopita katika
himaya yake ya kwanza kama Kocha .
Dunga alirudi tena kama Kocha wa Brazil Mwaka Jana baada ya Fainali
za Kombe la Dunia na kuiongoza Brazil kushinda Mechi 11 na kufungwa
Mechi 2 kwenye Copa America hii na kuamsha hisia mbaya toka Nchini kwao.
Brazil ndiyo Nchi inayoshikilia Rekodi ya kutwaa Kombe la Dunia
mara nyingi baada ya kulibeba mara 5 ikifuatiwa na Italy na Germany
zilizotwaa mara 4 kila mmoja, Argentina na Uruguaya mara 2 kila mmoja
huku England, France na Spain zikitwaa mara 1 kila mmoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni