ZIDANE 'AWASTUA' MAN UNITED-LULU MNAYO MNAICHEZEA!
Man United ilimnunua Guillermo Varela, mwenye Miaka 22 ambae
alikuwepo Timu ya Taifa ya Uruguay iliyocheza Copa America Wiki
iliyopita, Mwaka 2013 kwa Dau la Pauni Milioni 2 kutoka Klabu ya Penarol
ya Uruguay na kumsainisha Mkataba wa Miaka Mitano.
Varela, ambae ni Fulbeki wa Kulia, alichezea Kikosi cha Vijana wa
Man United cha U-21 na alipotua Louis van Gaal Mwaka Jana, Kijana huyo
akaruhusiwa kwenda kwa Mkopo huko Castilla baada ya Zinedine Zidane
kuvutiwa nae.
Zidane amezungumza: "Nilijua yupo Fulbeki wa Uruguay Man United.
Niliomba kumwona na nikampenda. Kwa bahati tuliweza kumleta Real Madrid
na naona atafaa sana hapa kwetu."
Maendeleo ya Varela sasa yamemgusa Louis van Gaal ambae anataka
kumchukua Kijana huyo kwenye Ziara ya huko Marekani ambako watakwenda
Julai 14 ili kumpima kama anaweza kuchukua namba ambayo sasa inachezwa
na Winga Antonio Valencia badala ya Rafael ambae kila Siku kaumia.
Tangu astaafu Fulbeki wa Kulia Gary Neville Februari 2011, Man
United haijapata Mtu barabara kwenye nafasi hiyo na imelazimika kumtumia
kiraka Valencia ambae ni mzuri kwenda mbele ila kwenye Difensi ni
dhaifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni