BARCA NA JUVE ZAKUTANA KUHUSU POGBA!
Vyanzo vya habari hizo, likiwemo La Gazzetta dello Sport la huko
Italy, vimedai Mkurugenzi wa Juve, Beppe Marotta na Msimamizi stadi wa
Uhamisho wa Barca, Ariedo Braida, walikutana Mjini Milan, Italy.
Ajenda ya Mkutano huo ilikuwa ni moja tu na nayo ni kujadili Uhamisho wa Pogba kutoka Juve kwenda Barca.
Suala la kumchukua Paul Pogba kwenda kuchezea Barca limekuwa moja
ya Ilani za Uchaguzi wa Rais wa Barcelona ambao Rais wa sasa Josep Maria
Bartomeu anachuana na Rais wa zamani Joan Laporta ambae yeye ameweka
suala la kumnasa Pogba ndio silaha yake wakati wa Kampeni za Uchaguzi
huo.
Hata hivyo La Gazzetta dello Sport limesema haijalishi nani atakuwa
Rais wa Barca kwani wote Bartomeu na Laporta wanamtaka Kijana huyo
anaechezea pia Timu ya Taifa ya Ufaransa.
Licha ya Manchester City kumtaka Pogba, Mchezaji wa zamani wa Timu
ya Vijana ya Mahasimu wao Man United, Barcelona ndio wanaodhaniwa
watamnasa kwani hilo ndio chaguo binafsi la Pogba.
Lakini pia manufaa kwa Juve kufanya biashara na Barca ni kuwa hata
Pogba akiuzwa sasa itabidi abakie Juve kwa vile Barca wapo kwenye
Kifungo cha kutonunua Wachezaji hadi 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni