MAN UNITED: JONES ASAINI MPYA, WACHEZESHA KAMARI WAFUNGA OFISI KUHUSU SCHNEIDERLIN KUJIUNGA!
MKATABA MPYA
Phil Jones, mwenye Miaka 23, amesaini Mkataba mpya na Man United
ambao utambakiza Klabuni hapo hadi Juni 2019 pamoja na nyongeza ya Mwaka
mmoja juu yake.
Jones alianza kuichezea Man United Mwaka 2011 na ameshacheza Mechi
128 na kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara moja Mwaka 2013.
Akiongea baada ya kusainiwa Mkataba huo mpya, Meneja Louis van Gaal
alisema: "Tumefurahi Phil amesaini Mkataba mpya. Yeye ni Mchezaji
mwenye kipaji anaeweza kucheza nafasi nyingi. Bado ni Kijana anae
endelea wakati wote."
Nae Phil Jones ameeleza: "Nimefurahishwa kusaini dili mpya. Hii ni Klabu kubwa kushiriki nayo na naungoja kwa hamu Msimu mpya."
BETI ZA SCHNEIDERLIN KUJIUNGA
Huku kukiwa na habari kuwa Kiungo wa Southampton Morgan
Schneiderlin atajiunga na Manchester United Jumatano Julai 1 wakati
Dirisha la Uhamisho litakapofunguliwa rasmi, Wachezesha Kamari
wamesimamisha kupokea Beti za Mchezaji huyo kama atajiunga na Man United
au la na hii ni dalili kubwa kuwa Uhamisho huo una uhakika.
Schneiderlin, Mchezaji wa Kimataifa wa France alieng'ara mno na
Southampton katika Misimu Miwili iliyopita, amekuwa akiwindwa pia na
Arsenal lakini inaelekea imebwaga manyanga.
Katika Siku za nyuma, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ashawahi
kuulalamikia mkono wa Manchester United katika Uhamisho wa Wachezaji kwa
kudai: "Kila Mchezaji anaeletwa kwangu, Manchester United wanakuwa
tayari washafika!"
Imeripotiwa kuwa Man United na Southampton zimeshakubaliana Ada ya
Uhamisho ya Pauni Milioni 25 kwa ajili ya Schneiderlin mwenye Miaka 25
ambae nae ashaafikiana kuhusu Maslahi yake binafsi ikiwemo kuzoa
Mshahara wa zaidi ya Pauni 100,000 kwa Wiki.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni