Brazil
imepata ushindi wake wa kwanza kwenye mashindano ya Copa America bila
ya nyota wake Neymar ambaye usiku wa jana alikuwan jukwaani kama
mshangiliaji wakati timu yake inakipiga dhidi ya Venezuela kwenye mchezo
wa mwisho wa kundi C ambapo Brazil ilishinda kwa goli 2-1 na
kujihakikishia kutinga kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Ilibidi
Neymar awe jukwaani kuishangilia timu yake kufuatia kulimwa kadi
nyekundu na kufungiwa kucheza mechi nne pamoja na faini ya dola 10,000
za kimarekani baada ya kuonesha utovu wa nidhamu kwa kumpiga na mpira
mchezaji wa Colombia na kumtolea mwamuzi maneno makali.
Thiago
Silva aliyenyang’anywa unahodha wa Brazil alianza kuifungia Brazil goli
la kwanza zikiwa zimepita dakika tisa tu tangu kuanza kwa mchezo,
lakini dakika ya 51 Roberto Firmino akaihakikishia Brazil kufuzu kucheza
hatua ya robo fainali baada ya kuifungia timu yake goli la pili
akimalizia kazi safi iliyofanywa na Wllian.
Goli
la kufutia machozi la Venezuela lilifungwa na Miku dakika ya 84 ya
mchezolakini lilikua halina msaada kwa timu yake ambayo imemaliza
mkiani kwenye kundi C ikiwa na ponti tatu.
Brazil itakutana na Paraguay
kwenye mchezo wake wa robo fainali utakaopigwa siku ya Jumamosi mchezo
ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkali na wenyekuvutia.
Mchezo mwingine wa kundi C
uliopigwa jana usiku ulikuwa kati ya Colombia dhidi ya Peru, mchezo huo
ulimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya bila kufungana ambapo Falcao
bado ameonekana kushindwa kurejesha makali yake ya kupasia nyavu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni