amos anukia kutua Old Trafford
Ramos haelewi ni kwanini Madrid
wameanua kumruhusu aondoke wakati bado anamkataba wa miaka miwili na
klabu hiyo lakini akawaambia kwamba, iwapo naondoka Madrid basi sehemu
pekee anayotaka kwenda ni Manchester United.
Ramos aliyejiunga na Madrid
kitokea Sevilla mwaka 2005 ameshatwaa mataji yote kwenye mchezo wa soka
akianzia ngazi ya klabu hadi kwenye timu ya taifa.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 29
hana furaha kwenye klabu yake hasa kwa kitendo cha klabu hiyo kuamua
kumtimua aliyekuwa kocha wao Carlo Ancelotti lakini pia kitendo cha
Madrid kushindwa kumpa Euro milioni 10 kwa mwaka kwa ajlili ya kuboresha
mkataba mpya.
Ramos aliamini kwamba,
angeongezewa mkataba mwingine kwenye majira ya kiangazi ya msimu
uliopita baada ya kuifungia timu yake goli la kusawazisha dakika ya
mwisho kwenye mchezo wa fainali wa klabu bingwa barani Ulaya dhidi ya
Atletico Madrid na kuisaidia timu hiyo kunyakua taji hilo kwa mara ya 10
kwenye muda wa nyongeza.
Klabu ya Barcelona imelalamika
kuwa, ilipeleka ofa ya kutaka kumsajili Ramos lakini hawakujibiwa
chochote na Madrid, kitendo hicho kimemchukiza pia Ramos ambaye amesema
anapenda zaidi kukipiga kwenye ligi ya EPL hasa Old Trafford japo bado
anawindwa na Barcelona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni