tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

22 Juni 2015

COPA AMERICA: BRAZIL BILA NEYMAR YATINGA ROBO FAINALI, FIRMINO SHUJAA!

COPA-AMERICA15Brazil, wakicheza bila ya Kepteni wao Neymar aliefungiwa Mechi 4, wametinga Robo Fainali ya Copa America baada ya kuifunga Venezuela 2-1 hapo Jana huko Estadio Municipal Concepcion Mjini Concepcion Nchini Chile.
Ushindi huo umeipa Brazil ushindi wa Kundi C na sasa watacheza na Paraguay, waliomaliza Nafasi ya Pili toka Kundi B, katika Robo Fainali.
Bao za Brazil katika Mechi hii na Venezuela zilifungwa na Thiago Silva, Dakika ya 9, na Roberto Firmino, Dakika ya 51 wakati lile la Venezuela lilifungwa na Nicolas Fedor Miku katika Dakika ya 84.
Katika Mechi nyingine ya Kundi C, Colombia na Peru zilitoka 0-0 na zote kutinga Robo Fainali.
++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
KUNDI A
**Kila Timu imecheza Mechi 3
1 Chile Pointi 7
2 Bolivia 4
3 Ecuador 3
4 Mexico 2
KUNDI B
**Kila Timu imecheza Mechi 3
1 Argentina Pointi 7
2 Paraguay 5
3 Uruguay 4
4 Jamaica 0
KUNDI C
**Kila Timu imecheza Mechi 3
1 Brazil Pointi 6
2 Peru Pointi 4
3 Colombia 4
4 Venezuela 3 
**Timu 2 za Juu kila Kundi na Timu za 3 mbili Bora zitasonga Robo Fainali
++++++++++++++++++++++
Robo Fainali zitaanza kuchezwa hapo Jumatano kwa Mechi kati ya Mabingwa Watetezi Uruguay na Wenyeji Chile.
VIKOSI:
Brazil (Mfumo 4-2-3-1): Jefferson; Dani Alves, Thiago Silva, Miranda, Filipe Luis; Fernandinho, Elias; Willian, Coutinho, Robinho; Firmino.
Akiba: Neto, Marcelo Grohe, Fabinho, Marquinhos, David Luiz, Geferson, Casemiro, Fred, Douglas Costa, Everton Ribeiro, Diego Tardelli.
Venezuela (Mfumo 4-2-3-1): Baroja; Rosales, Tunez, Vizcarrondo, Cichero; Rincon, Seijas; Guerra, Arango, Vargas; Rondon.
Akiba: Hernandez, Farinez, Angel, Martinez, Acosta, Perozo, Murillo, Gonzalez, Lucena, Rivas, Miku.
REFA: Enrique Cáceres [Paraguay]
FIRMINO-SCORES-COPA
COPA AMERICA 
RATIBA/MATOKEO:
**Saa za Bongo
Alhamisi Juni 11
KUNDI A Chile 2 Ecuador 0
Ijumaa Juni 12
KUNDI A Mexico 0 Bolivia 0
Jumamosi Juni 13
KUNDI B Uruguay 1 Jamaica 0
KUNDI B Argentina 2 Paraguay 2
Jumapili Juni 14
KUNDI C Colombia 0 Venezuela 1
KUNDI C Brazil 2 Peru 1
Jumatatu Juni 15
KUNDI A Ecuador 2 Bolivia 3
KUNDI A Chile 3 Mexico 3
Jumanne Juni 16
KUNDI B Paraguay 1 Jamaica 0
KUNDI B Argentina 1 Uruguay 0
Jumatano Juni 17
KUNDI C Brazil 0 Colombia 1
Alhamisi Juni 18
KUNDI C Peru 1 Venezuela 0
Ijumaa Juni 19
KUNDI A Mexico 1 Ecuador 2
KUNDI A Chile 5 Bolivia 0
Jumamosi Juni 20
KUNDI B Uruguay 1 Paraguay 1
KUNDI B Argentina 1 Jamaica 0
Jumapili Juni 21
KUNDI C Colombia 0 Peru 0 
KUNDI C Brazil 2 Venezuela 1
ROBO FAINALI
Jumatano Juni 24
Chile v Uruguay (Saa 8 na Nusu Usiku)
Alhamisi Juni 25
Bolivia v Peru (Saa 8 na Nusu Usiku)
Ijumaa Juni 26
Argentina v Colombia (Saa 8 na Nusu Usiku)
Jumamosi Juni 27
Brazil v Paraguay (Saa 6 na Nusu Usiku)
NUSU FAINALI
Jumatatu Juni 29
RF1 v RF2 (Saa 8 na Nusu Usiku)
Jumanne Juni 30
RF3 v RF4 (Saa 8 na Nusu Usiku)
MSHINDI WA 3
Ijumaa Julai 3
(Saa 8 na Nusu Usiku)
FAINALI
Jumamosi Julai 4
(Saa 5 Usiku)

Hakuna maoni: