JEURI YA REAL, KIBURI CHA MAN UNITED-UNAMTAKA DE GEA, TUPE RAMOS!
Akiwa amebakisha Mwaka mmoja kwenye Mkataba wake na Man United,
David de Gea alipewa Mkataba mpya ulioboreshwa lakini akawa anasita
kuusaini na kuibuka ripoti kuwa anataka kurudi kwao Spain kuidakia Real
Madrid.
Wakati hilo likonekana halikwepeki Man United nao wakajibu mapigo
kwa kuripotiwa wakitaka dili yeyote ya David de Gea ihusishe na wao
kupewa Mchezaji na sasa Beki Sergio Ramos ndie ameibuka mlengwa.
Lakini habari za ndani ya Real zinadai Ramos hawezi kwenda kokote
kwa vile Mkataba wake wa sasa unaoisha 2017 una kipengele cha Real
kulipwa Euro Milioni 200 ikiwa atahama kabla Mkataba kwisha.
Vile vile, Real wanaamini wao watampata De Gea na Ramos hataenda
kokote kwa vile nia yake si kuhama bali ni kuboreshewa Mkataba wakati De
Gea anataka kuhama ili arudi kwao.
Hata hivyo, Real wanasemekana kukiri kuwa mambo ni magumu kwani Man United hawataki mazungumzo yeyote kwa wakati huu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni