CRISTIANO RONALDO HANA FURAHA NA AMANI NDANI YA REAL MADRID KWASABABU HII
Kutokana na ripoti za gazeti la AS limeandika kwamba mchezaji muhimu wa Real Madrid Cristiano Ronaldo hana furaha na amani ndani ya Real Madrid hivi sasa.
Sababu kubwa inayomfanya CR7 asiwe na amani na furaha ndani ya Real ni kutokana na club inavyowa-treat marafiki zake wa karibu Iker Casillas na Sergio Ramos.
Licha ya kuwa marafiki zake wa karibu ni kwamba wachezaji hao wameitumikia club hiyo kwa muda mrefu lakini kwa wakati huu Real inataka kwa kuwauza kwa utaratibu ambao wote wawili hawafurahii. Cassilas anaonekana kachoka anatakiwa kubadilishwa na De Gea pamoja na dau la pesa.
Pia Ramos pia mambo yake sio mazuri. Cristiano Ronaldo hafurahii yanayotokea na kikubwa zaidi anahofia na yeye siku moja yasije kumtokea kama haya yanayowatokea wenzake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni