Mahakama yamfungia Jose Mourinho miezi sita
MENEJA
wa Chelsea,Jose Mourinho amefungiwa kuendesha gari kwa miezi sita kaaba
ya kutiwa hatiani kwa kosa la kuzidisha mwendokasi alilolifanya mwaka
jana.
Mwezi
septemba 2014, Mreno huyo aliripotiwa kunaswa na Camera akiendesha kwa
mwendokasi wa 60mph badala ya 50mph unaotakiwa katika ukanda A3 Esher
bypass, mjini Surrey.
Kesi
hiyo imesikilizwa jana katika mahakama ya Staines Magistrates na kocha
huyo mwenye miaka 52 ameamuriwa kulipa faini ya paundi 910 kwa
kuendesha kwa mwendokasi uliozidi 10pmh zaidi ya ule unaohitajika.
Pia anatakiwa kulipa faini ya paundi 750 na 75 ikiwa ni gharama za mahakama.
Hata hivyo, Mourinho hakuhudhuria mahakamani, lakini amekutwa na hatia baada ya kesi yake kusikilizwa.
Klabu ya Chelsea imekataa kutoa tamko baada ya kutafutwa kueleza hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni