Manchester United yafikia makubaliano na Real Madrid juu ya dili hili…
Casillas (kulia) anaondoka kumpisha De Gea (kushoto)
Klabu za Manchester United na Real Madrid zimekubaliana kufanya dili la golikipa wa Old Trafford, David de Gea.
Kwa
maana hiyo Iker Casillas anakaribia kuondoka Real Madrid kumpisha De Gea
kuwa kipa namba moja mara tu ataposaini mkataba wa kutumika Bernabeu
wiki ijayo.
De
Gea atakamilisha uhamisho wake kwenda Hispania baada ya kumaliza
majukumu ya timu ya taifa Jumapili hii na atakapotua Real Madrid,
Casillas ataondoka klabuni hapo baada ya kudumu kwa miaka 16.
Casillas
ambaye ameweka historia kubwa Real Madrid amebakiza miaka miwili katika
mkataba wake wa sasa na anataka kulipwa fidia yote endapo anatimka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni