MAMBO YANAKARIBIA KUKAMILIKA…BAADA YA DAU LA 50MIL, STERLING AKATISHA HOLIDAY AKODI NDEGE KURUDI UINGEREZA
Mchezaji Raheem Sterling wa Liverpool, amekatisha ziara yake ya mapumziko ‘bata’ huko Ibiza na kukodi ndege binafsi kurudi nyumbani Uingereza haraka huku Manchester City wakijiandaa kuongeza dau ili wamsajili.
Liverpool wamekataa dau la paundi 40m kutoka kwa Manchester City baada ya awali kukataa ofa ya paundi 30m kwa mchezaji huyo.
Habari kutoka Uingereza zinasema Manchester City wanafanya kila liwezekanalo kupata saini ya kijana huyo ambaye Liverpool wamekomaa kwamba ana thamani ya paundi 50m.
Raheem alionekana kufurahia maisha huko Ibiza wiki iliyopita lakini amerejea haraka nyumbani (uingereza) kwa ndege ya kukodi.
Wakati huo huo mlinzi wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Rio Ferdinand ameponda uhalisia wa thamani za wachezaji wa kiingereza. Ferdinand kupitia twitter yake binafsi aliandika kuonesha kutoridhishwa na thamani ya Harry Kane (paund 40m) pamoja na Sterling (paund 50m)
Wakati Sergio Aguero alinunuliwa kwa paund 38m na Alexis Sanchez paund 32m.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni