tecno

tecno

airtel

airtel

.

.

nido

nido

RADIO LISTEN NOW

11 Juni 2015

Mchezaji wa zamani wa Brazil ataka mikoba ya Blatter FIFA

ZiccoHuku kukiwa bado hali si shwari ndani ya shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Zico amepania kugombea urais wa shirikisho hilo baada ya kukiri kufadhaishwa na janga la rushwa katika uongozi wa FIFA.
Zico mwenye miaka 52 na ambaye jina lake halisi ni Arthur Antunes Coimbra amesema, ni wajibu wake kugombea. Akizungumza na kundi kubwa la waandishi wa habari katika kituo chake cha kufundisha soka huko mjini Rio de Janerio, Zico amesema ni huzuni kwenye michezo kuona kile kinachotokea katika soka leo hii. Kuona rushwa, lakini pia kuona uchapakazi unaofanywa na baadhi ya watu wazuri ukipotezwa. Pia aliongeza kuwa, ni wajibu wake sasa kutumia uzoefu na ujuzi wake kujaribu kugombea nafasi ya urais.
Hivi karibuni rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter, alitangaza kuwa atajiuzuru wadhifa wake huo ikiwa ni siku nne tu baada ya kuchaguliwa tena kushika madaraka hayo. Uamuzi huo wa Blatter ulikuja ikiwa ni siku chache tu baada mamlaka ya Marekani na Uswiz kufungua kesi ya rushwa kwa baadhi ya maafisa wa ngazi za juu kwenye shirikisho la FIFA.

Hakuna maoni: