Video: Real Madrid washangilia kuwa timu inayoongoza kutwaa mara nyingi tuzo ya Pichichi
Real Madrid imeshindwa kutwaa kombe lolote msimu wa 2014/2015, wakati wapinzani wao wakubwa, FC Barcelona wametwaa makombe matatu, La Liga, Copa del Rey na Uefa Champions League.
Hata hivyo, Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya ufungaji bora ya La Liga, Pichichi, na hiyo inakuwa tuzo ya 27 katika historia ya Real Madrid na kuwa timu iliyofanikiwa zaidi kwa wachezaji wake kupata mafanikio binafsi ya ufungaji.
Video hii hapa chini inaonesha Real Madrid wakishangilia kutawala tuzo ya Pichichi ambayo inaweza kuwashtua Barcelona.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni