Sio bure: Daktari afichua siri ya mafanikio ya Lionel Messi
Nyota wa klabu ya soka ya
Barcelona, Muargentina Lionel Messi aliachana na vyakula vya kisasa vya
dukani ‘super market’ na kuamua kutumia vyakula vya asili.
Daktari wa mchezaji huyo bora
mara nne wa dunia, Giuliano Poser amethibitisha kuwa ilibidi kufanya
mabadiliko ya chakula ili kumrudisha kwenye fomu yake ya zamani mchezaji
huyo.
Itakumbukwa kuwa Lionel Messi
alipoteza mara mbili mfululizo tuzo ya uchezaji bora wa dunia, Ballon
D’or kwa mpinzani wake wa muda mrefu Cristiano Ronaldo baada ya kutokuwa
na uwezo wake mzuri wa awali.
Pamoja na klabu yake ya Barcelona
kutofanya vizuri ndani ya misimu hiyo miwili mfululizo, pia Messi
alishindwa kuisaidia timu yake ya taifa ya Argentina ilipofungwa 1-0
dhidi ya mabingwa wa sasa wa dunia Ujerumani kwenye mechi ya fainali ya
kombe la dunia la FIFA nchini Brazil mwaka jana.
Inaelezwa kuwa baada ya kuanza
vibaya msimu huu uliomalizika kwa Barcelona kushinda vikombe vyote
vitatu walivyoshiriki ‘treble’ Lionel Messi alimtafuta daktari huyo
Giuliano Poser ambaye aliwahi kumsadia mwaka 2008 alipokuwa na matatizo
ya kiafya.
Poser anasema, “mara baada ya
kombe la dunia, kila kitu kilibadilika kwa Messi” amezungumza daktari
huyo wakati akiongea na gazeti la Delo Sport la Hispania.
“Messi ni kijana mpole na mtulivu. Hakuwa vizuri na akahisi kuna kitu kinahitaji mabadiliko” Poser anaeleza
Barcelona walianza kwa kususua
msimu huu na hata kupelekea mikwaruzano baina ya wachezaji na kocha wao
Jose Enrique, lakini mambo yalibadilika ghafla na kushuhudia wakirudi
katika mstari na fomu ya Messi ikawa ndio chachu ya wao kumaliza na
vikombe vyote walivyoshiriki msimu huu.
“Alibadilisha chakula, hatumii
tena vyakula vya dukani. Anakula vyakula vyenye utajiri wa vitamin,
madini, mbogamboga na maziwa.” Anamalizia Poser daktari wa mchezaji
huyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni