STRAIKA AMBAYE THIERY HENRY ALIMSHAURI ARSENE WENGER AMSAJILI ATUA ATLETICO MADRID
Atletico
Madrid imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa FC Porto,
Jackson Martinez, hii ni kwa mujibu wa wakala wa straika huyo wa
Colombia.
Martinez, 28, ambaye aliripotiwa kuwepo kwenye rada za Arsenal na AC Milan amekubali kutua Atletico kwa dau la Euro milioni 35.
“Dili limekamilika leo,”
amesema Wakala Luiz Henrique Pompeo na kuongeza: “Tunaishukuru AC Milan
kwa kuonesha nia toka mwanzo mpaka mwisho, tunajisikia kuheshimika,
lakini huwezi kucheza sehemu mbili kwa wakati mmoja”
Siku za karibuni, Gwiji wa zamani wa Arsenal, Thiery Henry alimshauri Arsene Wenger amsajili Martinez.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni