HII NDIO TAARIFA MPYA YA CHELSEA KUHUSU PAUL POGBA…
Kiungo wa Juventus, Paul Pogba
yupo kwenye rada za klabu kubwa barani ulaya ikiwemo Chelsea ambayo
imeingia rasmi katika mbio hizo jana.
Kwa mujibu wa Mwandishi maarufu
wa Italia, Gianluca Di Marzio, Chelsea wameshaanza kuwasiliana na Pogba
kuangalia uwezekano wa kumsajili.
Real Madrid, Barcelona, PSG na
Manchester City zinahusishwa kuiwinda saini ya nyota huyo kijana wa
Vibibi vya Turin na kama atasajiliwa kuna uwezekano wa kuwa mchezaji
ghali zaidi wa wakati wote duniani.
Kutokana na kukosa nafasi ya kucheza Old Trafford, Paul Pogba aliondoka Manchester United na kutua Seria A mwaka 2012.
Jose Mourinho tayari ana kiungo
mahiri wa kati, Nemanja Matic na kama wazo la kumsajili Paul Pogba
litakamilika, watatengeneza muunganiko wa hatari zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni