TAARIFA MPYA KUHUSU PETR CECH KUTUA ARSENAL ZATOKA….
Mashabiki wa Arsenal wamechoka
kusikia tetesi inayotangaza kwamba watamsajili golikipa wa Chelsea, Petr
Cech, lakini siku ya kufanya hivyo haijulikani.
Kwa wiki kadhaa, taarifa zimekuwa zikitoka kuwa Cech anaweza kusaini leo, lakini hiyo leo haifiki………..
Ijumaa iliyopita, Sky Sports walidai kwamba Cech angesaini Emirates siku hiyo, lakini haikutokea.
Hii inazua wasiwasi kama kweli Cech atajiunga na Arsenal majira haya ya kiangazi kwa dau la paundi milioni 11.
Hata hivyo, Jose Mourinho
hapendi kuona kipa huyo anajiunga na wapinzani wake wa ligi kuu England,
lakini mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich amemruhusu Cech kuondoka na
amemshukuru kwa kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio.
Leo kuna Tweet moja kutoka kwa
mwandishi wa gazeti la Dail Telegraph, Jason Burt akithibitisha kwamba
Cech atajiunga na Arsenal kesho Jumatatu, lakini baadhi ya watu
wamemjibu …
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni